Sinopsis
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.
Episodios
-
Waasi wa M23 huko DRC wajiimarisha katika kutengeneza serikali mbadala
07/10/2025 Duración: 10minWaasi huko mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wameendelea kujiimarisha kiutawala, kisiasa na kimiundo mbinu katika kujenga barabara, kutangaza orodha ya mawakili, hatua inayodhihirisha kuwa waasi hao wanaendea kutengeneza serikali mbadala na ile ya Kinshasa. Makala ya habari rafiki inaangazia hatua hiyo
-
Rais mstaafu wa DRC Joseph Kabila ahukumiwa kifo, maoni ya wasikilizaji
01/10/2025 Duración: 10minMahakama ya kijeshi nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC imemhukumu rais mstaafu wa nchi hiyo Joseph Kabila Kabange adhabu ya kifo bila ya yeye mwenyewe kuwepo mahakamani, ikimtia hatiani kwa usaliti na uhalifu dhidi ya binadamu. Chama chake PPRD kimesema kesi hiyo ni ya kisiasa dhidi ya mpinzani mkubwa wa serikali. Mwandishi wetu Ruben Lukumbuka anaungana na wasikilizaji wa Idhaa kupata maoni yao kuhusu kesi hii, makinika kwa kusikiliza makala hii.-
-
Serikali ya DRC kusitisha leseni za makanisa na taasisi za kisheria
30/09/2025 Duración: 10minSerikali ya DRC kupitia wizara ya sheria imesitisha utoaji wa leseni za Makanisa, katika kupambana na Rushwa! kwa maoni yako unaamini kusitisha utoaji wa leseni kutasaidia kupambana na rushwa? Hali ya rushwa ikoje katika taasisi za umma nchini mwako? Mwandishi wetu Ruben Lukumbuka pamoja na wasikilizaji wetu wanajaribu kupata jibu kwa maswali hayo
-
Tume ya uchaguzi nchini Kenya yazindua zoezi la uandikishaji wapiga kura
30/09/2025 Duración: 10minMakala ya habari rafiki ya jumatatu septemba 29 2025 imeangazia hatua ya tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC kuzindua zoezi la kuwaandika wapiga kura ambalo limeonekana kuwavutia vijana wengi, maarufu kama Gen Z.Tumekuuliza msikilizaji je? unaona vijana wote wako tayari kujiandikisha na katika nchi yako vijana wanahamasishwa vipi. Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka, kwa kutuma maoni ya sauti kupitia nambari yetu ya whatsApp: +254110000420 ama pia kupitia Facebook : RFI Kiswahili
-
Kila Ijumaa unachangia chochote ndani ya rfi Kiswahili
12/09/2025 Duración: 09minKila Ijumaa rfi kiswahili inakupa nafasi ya kuchangia mada yoyote, iwe kila kinaendelea hapo ulipo au yale umeskia kwenye matangazo yetu. Skiza maoni ya juma hili
-
Ethiopia yazindua bwawa lake la kuzalisha umeme
12/09/2025 Duración: 09minJe mataifa ya Africa yanatumia raslimali zake kujinufaisha? Skiza maoni ya wakilizaji
-
Kenya: Uporoja wa pesa za bima afya kizungu mkuti
10/09/2025 Duración: 09minShaba yetu inalenga Nchini Kenya, ambapo madai ya kupora kwa pesa za bima ya afya ya serikali yanaendelea kutatiza utowaji wa huduma ya afya hili likiwaathiri raia wa kawaida. Mskilizaji nchini mwako huduma za afya ni nafuu na bora, au bado wananchi wa kawaida wanahangaika kupata matibabu. Skiza maoni ya waskilizaji wetu
-
Umoja wa mataifa umesalia kimya ukiukaji wa haki ukiendelea
10/09/2025 Duración: 09minJe umoja wa mataifa umesalia kimya ukiukaji wa haki ukiendelea? Skiza makala haya kuskia hisia za waskilizaji wetu.
-
Raia wa nchi za Afrika wapendekeza watu wazima kupewa fursa ya kusoma na kuandika
10/09/2025 Duración: 09minKila mwaka tarehe 8 Septemba ulimwengu husherehekea maendeleo katika ujuzi wa kusoma na kuandika katika ngazi ya kimataifa, kikanda na kitaifa. Mwaka huu imekuwa ni fursa ya kutafakari kwa kina kuhusu maana ya kusoma na kuandika katika enzi hii ya kidijitali.
-
Kenya na Uganda zakubaliana rasmi kuondoa vizuizi vyote vya kibiashara
04/09/2025 Duración: 10minTunazungumzia hatua ya Kenya na Uganda kukubaliana rasmi kuondoa vizuizi vyote vya kibiashara, vikiwemo vizuizi vya ushuru na visivyo vya ushuru, ili kuwezesha mtiririko huru wa bidhaa, huduma, na watu kati ya mataifa hayo mawili
-
Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Tanzania zimeanza, wagombea wakinadi sera zao.
04/09/2025 Duración: 09minKampeni za uchaguzi mkuu wa Tanzania utakaofanyika tarehe 29 Oktoba zimeanza. Chama kikuu cha upinzani Chadema hakipo kwenye kampeni hizi, kufuatia msimamo wake wa kutaka mageuzi kwenye mfumo wa uchaguzi. Wasikilizaji wetu wanazungumzia aje kampeni hii na raia wa Tanzania wanatarajia sera gani kutoka kwa viongozi mbalimbali?
-
CHAN 2025: Nchi gani ilipendeza wasikilizaji wetu na maandalizi yalikuwa aje?
04/09/2025 Duración: 09minMichuano ya CHAN imemalizika rasmi mwishoni mwa juma, nchini Kenya, Morocco wakitawazwa mabingwa na Madagascar wakimaliza wa pili. Kuisha kwa michuano hii ni mwanzo wa maandalizi ya michuano ya AFCON itakayofanyika tena kwenye nchi za Kenya, Uganda na Tanzania mwaka 2027. Tumemuuliza msikilizaji wetu iwapo amefurahia michuano ya mwaka huu? Timu ipi ilikuwa bora kwake na kipi kifanyike kuelekea mashindano ya AFCON 2027.
-
-
-
Miaka kumi na mitano tangu Kenya kupata katiba mpya ambayo imetajwa endelevu
29/08/2025 Duración: 09min -
Mapigano kati ya FARDC na waasi wa M23 yanaendelea licha ya makubaliano ya amani
27/08/2025 Duración: 09min -
Je timu za nchi wenyeji wa CHAN zimefanyaje kwenye mchuoano wa CHAN 2024?
26/08/2025 Duración: 10minTimu za Kenya Uganda na Tanzania zimeaga mchuano katika hatua ya robo fainali
-
Michuano ya CHAN inaendelea je umeridhishwa kufikia sasa
23/08/2025 Duración: 10minMichuano ya CHAN inaendelea kuchezwa je umeridhishwa na michezo hiyo hadi kufikia sasa Skiza maoni ya mskilizaji.
-
Tanzania : Yabuni sheria kuwafungia nje wafanyakazi wageni
22/08/2025 Duración: 09minNchini Tanzania, nchi hiyo imebuni sheria kuwafungia nje wafanyakazi kutoka mataifa ya nje. Waskilizaji wetu walikuwa na haya ya kusema Skiza makala
-
Asasi za kiraia zamtaka rais William Ruto kuwataja hadharani wanaopokea rushwa
22/08/2025 Duración: 09minRais wa Kenya William Ruto, yupo kwenye shinikizo kubwa za kuwataja hadharani wabunge na Maseneta, aliodai wanapokea rushwa kutoka kwa Mawaziri na Magavana, asasi za kiraia zinasema hiyo ndio njia pekee ya kuwaaminisha wananchi kuwa, kiongozi huyo ana nia ya kupambana na ufisadi nchini humo.