Habari Rfi-ki

Rais mstaafu wa DRC Joseph Kabila ahukumiwa kifo, maoni ya wasikilizaji

Informações:

Sinopsis

Mahakama ya kijeshi nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC imemhukumu rais mstaafu wa nchi hiyo Joseph Kabila Kabange adhabu ya kifo bila ya yeye mwenyewe kuwepo mahakamani, ikimtia hatiani kwa usaliti na uhalifu dhidi ya binadamu. Chama chake PPRD kimesema kesi hiyo ni ya kisiasa dhidi ya mpinzani mkubwa wa serikali. Mwandishi wetu Ruben Lukumbuka anaungana na wasikilizaji wa Idhaa kupata maoni yao kuhusu kesi hii, makinika kwa kusikiliza makala hii.-