Habari Rfi-ki

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 3:59:12
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.

Episodios

  • Kenya: Yawarejesha nyumbani raia wake waliotapeliwa kuenda Mynamar

    08/04/2025 Duración: 09min

    Shaba yetu kwenye makala haya inalenga hatua ya Serikali ya Kenya, kueeendelea kuwarejesha mamia ya raia wake waliotapeliwa na kusafirishwa hadi nchini Myanmar kwa ahadi ya kupewa ajira.  Nchini mwako visa kama hivi vinaripotiwa?Ndilo swali letu, skiza makala haya kuskia baadhi ya maoni ya waskilizaji.

  • Africa Mashariki : Viongozi watathimini kudhibiti mitandao ya kijamii

    08/04/2025 Duración: 09min

    Katika makala haya tunajadili haja ya kuwepo sheria za kudhibiti mitandao ya kijamii kwa baadhi ya mataifa ya Africa Mashariki. Skiza makala haya kuskia mano ya waskilizaji wetu.

  • Maoni ya waskilizaji kuhusu wizi unaofanywa kwenye mizani na wafanyabiashara

    05/04/2025 Duración: 10min

    Makala haya ni maoni ya waskilizaji kuhusu ripoti maalum ya namna wananchi wanavyopigwa na wafanyabiashara kwenye mizani wanapopimiwa nafaka mbalimbali za chakula, huku gesi ya kupikia pia ikitajwa.

  • Maoni yako kwenye makala ya Habari Rafiki Mada Huru Ijumaa

    28/03/2025 Duración: 10min
  • DRC: Majadiliano ya kitaifa kuhusu kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa kitaifa

    25/03/2025 Duración: 10min
  • Qatar : Yakutanisha Kagame na Tshisekedi

    20/03/2025 Duración: 09min

    Shaba yetu  leo kwenye makala haya inalenga taifa la Qatar ambapo taifa hilo juma hili lilifanikiwa kuwaleta pamoja marais Felix Tshiesekedi wa DRC na mwenzake wa Rwanda Paul Kagme, katika juhudi za kutafuta suluhu kwa mzozo wa mashariki ya DRC. Unafikiri Qatar itafanikiwa kuzima mzozo wa mashariki mwa DRC. Skiza makala haya kujua baadhi ya maoni ya waskilizaji.

  • Kenya : Kanisa katoliki latangaza marufuku kwa wanasiasa

    19/03/2025 Duración: 10min

    Tunajadili  hatua ya Kanisa la Anglikana nchini Kenya, kwa mara nyingine limesisitiza marufuku ya kuwazuia wanasiasa kuzungumza kanisani katika juhudi za kuzuia wanasiasa kufanya siasa kanisani. Je unazungumziaje hatua hii ya kanisa Anglikana nchini Kenya? Skiza makala haya kuskia baadhi ya maoni ya waskilizaji wetu.

  • Rwanda yasitisha uhusiano na Ubelgiji

    18/03/2025 Duración: 09min

    Katika makala haya tunajadili hatua ya serikali ya Rwanda, kutangaza kusitisha uhusiano wa Kidiplomasia na taifa la Ubelgiji kutokana na kile Rwanda imesema Ubelgiji kuendeleza propaganda kuihusu kutokana na mzozo wa mashariki mwa DRC. Unazungumziaje hatua ya Rwanda Skiza makala haya kuskia baadhi ya maoni ya waskilizaji.

  • Watu zaidi ya milioni 6 duniani watakosa mahali pakuishi

    17/03/2025 Duración: 10min

    Tunajadili hatua ya bazara la wakikimbizi la Denmark, kuchachapisha ripoti inayoonesha kuwa, watu zaidi ya milioni 6 duniani watakosa mahali pakuishi ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao, kutokana na mizozo, mabadiliko ya tabia nchi na kusitishwa kwa misaada toka Marekani. Unazungumziaje hatua hii? ndilo swali tumeuliza, skiza makala haya kufahamu mengi.

  • Maoni yako kutokana na habari zetu juma hili

    14/03/2025 Duración: 10min

    Kila Ijumaa rfi Kiswahili inatoa nafasi kwa mskilizaji kuchaniua mada mbalimbali kuhusu taarifa zetu. Juma hili hizi ni haya ni baadhi ya maoni ya waskilizaji wetu

  • DRC : Angola kufanikisha mkutano kati ya rais Tshisekedi na waasi wa M23

    13/03/2025 Duración: 09min

    Shaba yetu inalenga nchini DRC, ambapo taifa la Angola limesema linajaribu kufanikisha mazungumzo ya moja kwa moja kati ya rais wa DRC, Felix Tshisekedi na waasi wa M23, ili kutafuta suluhu la mzozo wa mashariki mwa DRC. Je unafiriki Angola itafanikiwa katika hili?Haya hapa baadhi ya maoni yako.

  • Sudan Kusini :Wanajeshi wa Uganda wawasili Sudan Kusini

    13/03/2025 Duración: 09min

    Mkuu wa majeshi nchini Uganda, ambaye pia ni mwana wa rais Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba, amedai wanjeshi wa taifa lake wamewasili Sudan Kusini ili kusaidia jeshi la taifa hilo kutatua mzozo ndani ya serikali ya umoja wa kitaifa  Tunakuuliza je mzozo wa Sudan Kusini unastahili kutatuliwa kijeshi?Skiza makala haya kuskiza baadhi ya maoni yenu.

  • Kenya: Vijana wapinga michango ya wanasiasa kanisani

    11/03/2025 Duración: 09min

     Shaba yetu leoinalenga nchini Kenya ambapo Vijana wameanza kuandamana kupinga kile wanadai wanasiasa kutoa kiasi kikubwa cha pesa kwenye maeneo ya kuabudu ili hali wao hawana ajira. Tumekuuliza hatua hii ni sahihi?Haya hapa baadhi ya maoni yako.

  • Kenya : Rais Ruto na mpinzani Raila Odinga kushirikiana

    11/03/2025 Duración: 09min

    Mwishoni mwa juma  lililopita rais wa Kenya William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga walitiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kisiasa, wanaosema utasaidia kutatua changamoto  zinazowakabili raia wa taifa hilo.  Unaamini makubaliano ya viongozi hawa ni sahihi?Ndilo swali tumekuuliza na haya hapa maoni yako.

  • Hatua ya rais Donald Trump kusitisha msaada wakijeshi kwa nchi ya Ukraine

    06/03/2025 Duración: 10min
  • Maoni kuhusu vingozi wa kijeshi wa nchi za Afrika Magharibi kutaka kugombea urais

    05/03/2025 Duración: 10min

    Nchini Gabon, kiongozi wa kijeshi jenerali Brice Oligui Nguema ametangaza kuwa atagombea urais katika uchaguzi wa mwezi ujao, baada ya kutwaa madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi ya 2023.Hili linajiri wakati huu viongozi wengine wa kijeshi kwenye nchi za Burkina Faso, Mali na Niger wakielekea kuchukua mkondo huo.

  • Vyama vya upinzani nchini Uganda kufunga kuwaombea wafungwa wa kisiasa

    04/03/2025 Duración: 09min
  • Kila Ijumaa ni mada huru ambapo unatoa maoni kuhusu ulichokiona wiki hii

    28/02/2025 Duración: 10min

    Leo ni Ijumaa ,,siku ya mada huru kwenye habari rafiki  ambapo Tunakupa nafasi ya kuzungumzia suala lolote ambalo limetokea nchini mwako wiki hii au kile ambacho umekisikia kwenye matangazo yetu ya juma hili

  • Rais wa Uganda Yoweri Museveni asikitishwa na hali ya umaskini nchini mwake

    27/02/2025 Duración: 10min

    Mada  ni kuhusu..kauli ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni Akiwa katika ziara ya kawaida kuzungumza na raia wake , ameeleza kuguswa na kusikitishwa na hali ya umasikini anayoshuhudia kwenye nchi yake,,,wakati huu tatizo la umasikini linashuhudiwa pia kwenye mataifa mengine ya ukanda.Tulimuuliza mskilizaji  anazungumziaje kauli ya Rais Museveni na je viongozi wa ukanda wamefanya vyakutosha kupambana na umasikini?

  • Rais wa DRC, Felix Tschsekedi, atangaza kuunda Serikali ya umoja wa kitaifa

    24/02/2025 Duración: 10min

    Karibu  kwenye kipindi cha leo ambapo tunaangazia tangazo la  Rais wa DRC, Felix Tschsekedi, kuwa  ataunda Serikali ya umoja wa kitaifa, hatua inayokuja wakati huu akiwa katika shinikizo kutoka ndani na nje ya nchi yake, kuhusu namna alivyoshughulikia mzozo wa mashariki mwa nchi yake, wakati huu waasi wa M23 wakichukua miji zaidi.

página 1 de 2