Sinopsis
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.
Episodios
-
Mada Huru: Maoni kuhusu habari kuu wiki hii na matukio katika maeneo mbalimbali
21/02/2025 Duración: 09minIkiwa ni siku ya Ijumaa, ni wakati wa mada huru, yaani tunampatia mskilizaji nafasi kuchangia habari kuu ambazo tumekuwa nazo wiki hii hapa RFI Kiswahili au kutueleza jambo ambalo limetokea nchini mwake juma hili. Leo pia msikilizaji ni siku ya lugha mama, ningependa sana nikusalimie kwa lugha yako mama lakini ningependa kusikia kutoka kwako kwanza. Jambo!
-
Maoni: Marekani yaanza mazungumzo na Urusi ya kusitisha vita nchini Ukraine.
21/02/2025 Duración: 09minHaya ni makala ya Habari Rafiki tukiangazia maoni ya waskilizaji wa RFI Kiswahili kuhusu mada kwamba, Marekani imeanza mazungumzo na Urusi, lengo likiwa kupata mkataba wa kusitisha vita nchini Ukraine. Ukraine ambayo haijashirikishwa kwenye mchakato huo inasema haitakubali mkataba wowote bila kuhusishwa.Tumemuuliza msikilizaji je, Marekani inaweza kumaliza vita vya Ukraine? Na anafikiri ni kwanini Marekani haijaishirikisha Ukraine na mataifa ya Ulaya kwenye harakati hizi?
-
Wanamgambo wa RSF waandaa mkutano wa kuunda serikali mbadala Nairobi
19/02/2025 Duración: 10minWanamgambo wa RSF wanaopigana na jeshi nchini Sudan na washirika wake wakiwemo wanasiasa wapo jijini Nairobi nchini Kenya, wanakojadiliana kuhusu uundwaji wa serikali mbadala wakati huu inapoendelea na vita.Unazungumzia vipi harakati hizi za RSF ?Unafikiri ni kwanini Kenya imewaruhusu wanamgambo hao kukutana katika nchi yake ?
-
Kikao cha usalama wa DRC na Sudan chakamilika Ethiopia bila suluhu
17/02/2025 Duración: 10minMakala ya leo yanaangazia Kikao cha viongozi wa Afrika, kilichotamatika rasmi mwishoni mwa juma lililopita nchini Ethiopia, mzozo wa DRC na Sudan ukigubika mijadala yao.Hata hivyo vikao hivyo vimekamilika bila suluhu ya mizozo ya nchi zote mbili, ambapo vyongozi waliishia kwa kutoa wito wa kusitisha mapigano. tulimuuliza msikilizaji iwapo anaridhika na matokeo ya kikao hicho na anadhani nini cha zaidi viongozi hawa wangefanya kukomesha mizozo barani Afrika