Sinopsis
Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.
Episodios
-
Kenya : Ukeketaji bado changamato Africa
20/11/2025 Duración: 09minKatika maeneo ya wafugaji wa kuhamahama nchini Kenya, mila na desturi bado zinaonekana kupewa kipaumbele kuliko elimu – hali inayowafanya wasichana kuwa katika hatari kubwa ya kukeketwa. Wasichana wengi hukatizwa masomo na kulazimishwa kufuata tamaduni zinazokiuka haki zao, huku ukeketaji ukiendelea kufanywa kwa usiri mkubwa licha ya juhudi za serikali na wadau kutoa elimu na kupiga marufuku tendo hilo. Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa ukeketaji wa wasichana na wanawake wenye umri wa miaka 15 hadi 49 bado ni tatizo linaloripotiwa nchini Kenya. Katika makala haya tunaangazia namna tamaduni hizi zimeendelea kushamiri katika jamii za wafugaji wa kuhama hama na jinsi zinavyomnyima mtoto wa kike haki yake ya kupata elimu na kuishi bila unyanyasaji.
-
Matumizi ya hadithi kupigania haki
17/11/2025 Duración: 09minKatika makala haya tunangazia safari ya kutetea haki za binadamu kwa kutumia hadithi sauti moja, uzoefu, na ujasiri wa mtu kusimulia alichopitia. Tasisi ya Moth, imekuwa ikitumia hadithi kama si tu kwa mudhadha wa burudunai bali ni daraja linalounganisha ukweli wa mtu mmoja na uelewa wa dunia nzima. Hadithi nyingi ni za binafsi, lakini hisia zinazozibeba—hofu, matumaini, maumivu au ushindi—ni za ulimwengu mzima. Skiza makala haya kufahamu mengi.
-
Mila zanakandamiza wanawake nchini Kenya
17/11/2025 Duración: 09minMila na tamaduni kutoka jamii mbalimbali nchini Kenya, zimezidi kukandamiza wanawake kutoridhi mali. Pwani ya Kenya, changamoto hiyo pia imeathiri wanawake wajane skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.
-
-
DRC : Haki za raia wanaoishi na ulemavu Goma, DRC
25/10/2025 Duración: 09minKatika makala haya shaba yetu inalenga nchini DRC hasa eneo la Mashariki, ambapo tunajadili haki za malemavu eneo hilo. Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mamia ya watu wenye ulemavu wamejikuta wakihangaika kuokoa maisha yao, kipindi hiki vita vikiendelea kusheheni eneo hilo. Miji kama Goma, Rutshuru na Sake imeshuhudia maelfu wakikimbia maakazi yao. Lakini kwa wengi wenye ulemavu, kukimbia si jambo rahisi. Wengine wanatembea kwa magongo, wengine hutumia viti vya magurudumu ambavyo haviwezi kuvuka matope, milima, au mabonde. Skiza makala haya kufahamu mengi
-
Uganda : Uchaguzi raia wanafahamu haki zao
18/10/2025 Duración: 09minUchaguzi nchini Uganda, unatarajiwa kufanyika mwezi January, Rais Museveni akichuana tena na Hasimu wake wa kisiasa mwanamziki aliyeukia siasa, Bobi Wine. Skiza makala haya kufahamu mengi.
-
Kenya/Nigeria : Wanawake wanahangaishwa kwa mitandao
06/10/2025 Duración: 10minKatika makala haya tunaangazia suala linalozidi kuwa pasua kichwa—unyanyasaji wa wanawake kwenye mitandao ya kijamii. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na shirikisho la mawakili wanawake nchini Kenya FIDA, kwa ushirkiano na wenzao wa kutoka nchini Nigeria, unaonesha kuwa karibu kila mwanamke anayetumia mitandao amewahi kushambuliwa iwe ni kwa maneno ya matusi, vitisho, au kusambaziwa picha binafsi bila idhini yake. Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.
-
DRC : Unyanyasaji wa haki za watoto
05/10/2025 Duración: 09minWatoto wanatumika kwa baishara ya ngono Skiza makala haya kufahamu mingi zaidi
-
Kenya: Wayu Daba wapokeahati miliki ya shamba
23/09/2025 Duración: 10minKatika makala haya tunaangazia hatua ya kihistoria kwa jamii ya wafugaji nchini Kenya. Jamii ya Wayu Daba imekabidhiwa rasmi hati miliki ya ardhi yao kupitia Mpango wa Kusimamia Ardhi Kidigitali, unaoendeshwa na serikali mradi unaotekelezwa kwa ushirikiano na Shirika la Chakula na Kilimo, FAO. Hati hii inaguza maeneo makubwa ya ardhi, ikiwemo ardhi loevu yenye rutuba, misitu ya kiasili yenye wanyama na mimea adimu, pamoja na maliasili zinginezo ambazo zimekuwa nguzo ya maisha ya jamii hiyo kwa vizazi vingi Skiza makala haya kufahamu mengi.
-
Africa : Haki ya waandishi wa vitabu
19/09/2025 Duración: 10minKatika makala haya tutajadili haki za mwandishi wa vitabu, Je, mwandishi wa kitabu ana haki gani anapochapisha kitabu chake katika mashirika ya uchapishaji? Ni kipi kinafaa kuzingatiwa katika mchakato wa uchapishaji? Maswali haya yote yanamzunguka mwandishi, mchapishaji na shirika la uchapishaji ili kuibuka na mwafaka katika tasnia ya uandishi. Na ndiyo baadhi ya mambo yanayojadiliwa kwenye makala haya.
-
Maandiko matakatifu yapewe nafasi kusuluhisha mizozo
17/09/2025 Duración: 10minKatika makala haya tunaangazia safari ndefu ya amani katika mataifa yanayopitia migogoro, Shabaha ikiwa ni Sudan Kusini na Somalia. Mataifa haya yamepitia miongo kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, mizozo ya kisiasa, na changamoto za kiusalama ambazo zimeathiri mamilioni ya raia wao. Lakini katikati ya changamoto hizo, mashirika mbalimbali ya kimataifa na ya kikanda yamekuwa mstari wa mbele kusukuma gurudumu la amani. Skiza makala haya kufahamu mengi.
-
Mashambulizi kupitia mitandao ya kijamii
02/09/2025 Duración: 09minMitandao ya kijamii na teknolojia za kidijitali zimekuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Tunawasiliana, tunajifunza, tunafanya biashara na hata kushiriki mijadala ya kitaifa kupitia mitandao. Lakini pamoja na manufaa haya, kumekuwa pia na changamoto kubwa: mashambulizi ya maneno, udukuzi wa akaunti, na hata ulaghai wa kifedha. Skiza makala haya kufahamu mengi.
-
Je mchango wa wanawake ni upi katika juhudi za kupigania haki zao
29/08/2025 Duración: 09minWanawake wametuhumiwa kwa kukosa kupigania haki zao, lakini msimamo huu unakanusha na wengi. Skiza makala haya kufahamu mengi.
-
Dunia: watoto wanazidi kutumika kama vijakazi
23/08/2025 Duración: 10minMwezi wa Juni ulishuhudia matukio mawili muhimu ya kimataifa yakiangazia haki na ustawi wa watoto. Mnamo tarehe 12 Juni, dunia iliadhimisha Siku ya kupinga Ajira ya Watoto, (World Day Against Child Labor) ikirejelea takwimu za kutisha kwamba watoto milioni 160 duniani kote bado wamenaswa katika ajira ya watoto - wengi wakifanya kazi chini ya mazingira hatarishi. Skiza makala haya kufahamu mengi.
-
Africa : Mazingira yanavyoathiri haki za watoto
22/08/2025 Duración: 09minKatika makala haya tunangazia uharibifu wa mazingira unavyoathiri haki za watoto. Skiza makala haya kufahamu zaidi.
-
Kenya : Haki ya kumiliki ardhi ya jamii ya wafugaji
22/08/2025 Duración: 10minJamii za wafugaji nchini Kenya, bado zinapitia changamoto za kumiliki ardhi, jamii hizo ni kama vile,Turkana, Samburu, Rendille, Borana, Gabra na nyingine , zimeathiriwa kwa muda mrefu na unyang’anyi wa ardhi wakati wa ukoloni, ambao uliendelezwa hata baada ya uhuru . Licha ya kutambuliwa kwa haki za jamii katika Katiba ya 2010 na kupitishwa kwa Sheria ya Ardhi ya Jamii ya mwaka 2016, jamii hizi bado zinakumbwa na changamoto za ardhi,unyang’anyaji wa mashamba na ukosefu wa haki za kisheria—hali inayotishia siyo tu maisha yao bali pia utamaduni.
-
EAC : Uhuru na haki ya wanahabari kujiunga miungano
30/07/2025 Duración: 09minKataika makala haya tunajadili umuhimu wa wanahabari kuelewa na kulinda haki zao, hasa kupitia vyama na miungano ya waandishi wa habari. Katika mazingira ambapo uhuru wa habari uko mashakani, na waandishi wengi wanakumbwa na changamoto kazini, je, kuna msaada wowote wa pamoja? Ni moja tu ya maswali tunayatarajia kuyajibu kwenye makala ya haya. Skiza makala haya kufahamu mengi
-
EAC : Wakimbizi wazidi kukimbia makwao wakitafuta amani
28/07/2025 Duración: 10minMaelfu ya watu kote barani Afrika wanalazimika kuyahama makazi yao—wengine kwa sababu ya vita, wengine kwa sababu ya mateso au hali ngumu ya maisha. Wanakimbilia nchi jirani wakitafuta usalama, hifadhi, na matumaini ya kuanza upya, lakini safari ya kuwa mkimbizi si rahisi, ni safari ya maumivu, vizingiti, na kupoteza mengi. Katika makala haya tunajadili visingiti wanavyokumbana navyo watu wanaokimbia maakazi yao kutokana na vita. Skiza makala haya kufahamu mengi.
-
Kenya : Haki ya mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa
17/07/2025 Duración: 09minkatika makala haya mskilizaji tunazAma kuangazia uamuzi wa kihistoria uliofanywa hivi majuzi na Mahakama ya juu zaidi ya Kenya kuhusu haki za mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa ya dini ya Kiislamu—hasa kuhusu haki ya kurithi mali ya baba yake. Uamuzi huu umetangazwa kuwa hatua muhimu katika mapambano ya kuhakikisha kila mtoto anaheshimiwa na kulindwa kikatiba bila kujali dini au mazingira ya kuzaliwa kwake. Kwa miongo mingi, baadhi ya watoto waliozaliwa nje ya ndoa, hasa katika jamii za Kiislamu, wamekuwa wakinyimwa haki ya kurithi mali ya baba zao moja kwa moja kwa mujibu tamaduni ya dini hiyo. Kufamu mengi skiza makala haya.
-
Maziwa Makuu : Haki ya afya ya akili
15/07/2025 Duración: 10minAfya ya akili ni nguzo ya kila mmoja wetu ili kuafikia haki nyingine muhimu. Benson Wakoli alifanya mazungumzo na bi Ann Maria Qwicha, mwanahabari na mtetezi wa haki za binadamu hasa afya ya akili ili kufahamu mengi zaidi katika mapambano haya ya kuhakikisha afya ya akili inalindwa.