Jua Haki Zako

Informações:

Sinopsis

Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.

Episodios

  • Mashirika ya misaada ya kibinadamu yakumbwa na uhaba wa fedha

    19/12/2023 Duración: 09min

    Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR, limeonya kuwa mashirika ya misaada yanakabiliwa na uhaba wa fedha, na kwamba yanahitaji dola milioni 400 kufikia mwisho wa mwaka huu. Katika kongamano la siku tatu kuhusu wakimbizi huko Geneva, Wiki iliyopita, Mkuu wa shirika hilo Filippo Grandi, alisema asilimia 75 ya wakimbizi wanaishi katika nchi maskini na zile zinazoendelea.Grandi ameiomba jamii ya kimataifa kutofumbia macho mamilioni ya waliokimbia makazi yao huko Ukraine, Sudan, Syria, Afghanistan, na vile vile DRC.Kuzungumzia haya na pia haki za wakimbizi kwa ujumla, Bi. Faith Kasina, msimamizi wa UNHCR ukanda wa Afrika mashariki alizungumza na George Ajowi.

  • Ipo siku watu wanaoishi na walemavu watapata nafasi sawa katika jamii

    11/12/2023 Duración: 10min

    Tarehe 3 Disemba mwaka huu, dunia iliadhimisha Siku ya Kimataifa ya watu wanaoishi na ulemavu. Siku hii iliasisiwa mwaka 1992 na umoja wa mataifa. Nchini Kenya, siku hii ilifana sana huku sherehe ikiandaliwa katika maeneo mbalimbali. Katika eneo la Dagoreti, jijini Nairobi, tulikutana na Grace Wanjiku Maina ambaye alizaliwa na ulimavu lakini amejizatiti na kufanikiwa sana katika Jamii.Licha ya kuishi na Ulemavu Grace ni mshinda wa tuzo ya urembo ya kinadada wanaotumia vitu vya magurudumu, tuzo alioyoishinda 2017 na 2018, vile vile ni mwakilishi wa watu wanaoishi na ulemavu katika eneo la Dagoreti na pia mkurugenzi katika wakfu wa Sweet Aroma foundation, wakfu ambao unawatetea walemavu. Katika makala ya leo nimeanza kwa kumuuliza, nini kimebadilika tangu aliposhinda taji la urembo la miss Wheelchair miaka 6 iliyopita?

  • Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu kushinikiza serikali kutekeleza maamuzi ya mahakama

    04/12/2023 Duración: 10min

    Mtandao wa Taasisi za Kitaifa za Haki za Kibinadamu za Kiafrika (NHRI)kwa ushirikiano na Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KNCHR) pamoja na Taasisi ya Sheria ya Kibinadamu na Haki za Kibinadamu ya Raoul Wallenberg iliyo na makao yake makuu nchini Sweden iliandaa warsha ya kutathmini miradi kuhusu mafunzo ya Haki za Kibinadamu barani Afrika na ufuatiliaji wa jinsi ya Kutekeleza mapendekezo ya Maamuzi. Katika makala haya  Petronila Mukaindo, naibu mkurugenzi wa KNCHR anatoa twasira kamili ya changamoto na hatua za kutetea haki za kibinadamu nchini kenya na katika mataifa mengine.Kwa mengi zaidi skiza makala haya.

  • Siku 16 za mapambano dhidi ya ukatili wa wanawake

    01/12/2023 Duración: 10min

    Kila mwaka dunia hutumia  siku 16  kuadhimisha mapambano ya kupinga ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto . Umoja wa mataifa huongoza kampeni hii na hufanyika kuanzia tarehe 25 Novemba na kumalizika tarehe 10 Desemba ya kila mwaka kwa ajili ya kupinga ukatili na kutetea haki za wanawake.Siku hiyo ilianza kuadhimishwa rasmi mwaka 1991 na tangu wakati huo zaidi ya asasi 6,000 kwa  zaidi ya nchi 187 hushiriki katika maadhimisho haya. Nchini Kenya katika eneo la Kibra baadhi ya kinadada wamethibitisha kuwa visa vya dhulma bado vipo na kati ya wanawake 5 wawili wamedhulumiwa kisaikologia na hata kingono .Ili kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.

página 2 de 2