Jua Haki Zako
Kenya : Ukeketaji bado changamato Africa
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:09:56
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Katika maeneo ya wafugaji wa kuhamahama nchini Kenya, mila na desturi bado zinaonekana kupewa kipaumbele kuliko elimu – hali inayowafanya wasichana kuwa katika hatari kubwa ya kukeketwa. Wasichana wengi hukatizwa masomo na kulazimishwa kufuata tamaduni zinazokiuka haki zao, huku ukeketaji ukiendelea kufanywa kwa usiri mkubwa licha ya juhudi za serikali na wadau kutoa elimu na kupiga marufuku tendo hilo. Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa ukeketaji wa wasichana na wanawake wenye umri wa miaka 15 hadi 49 bado ni tatizo linaloripotiwa nchini Kenya. Katika makala haya tunaangazia namna tamaduni hizi zimeendelea kushamiri katika jamii za wafugaji wa kuhama hama na jinsi zinavyomnyima mtoto wa kike haki yake ya kupata elimu na kuishi bila unyanyasaji.