Jua Haki Zako

Kenya : Serikali yaanza kutoa miili ya waumini waliofariki baada ya kususia chakula ili wamuone Yesu

Informações:

Sinopsis

 Unamkumbuka  kiongozi wa wa dini Paul Mackenzi anayetuhumiwa kwa kushiwishi waumini wake kususia chakula hadi kufa, ili kukutana na yesu nchini Kenya. Baada ya takriban  mwaka moja na mwezi mmoja wa serikali ya Kenya kufukua miili ya waumini   waliofariki na kuzikwa katika msiku wa Shakahola na kuzifanyia uchuguzi wa vina saba yaani DNA, serikali sasa imeanza kutoa miili hiyo kwa familia za jamaa waliofariki.Serikali ya Kenya kupitia kwa mwanapatholijia wake mkuu daktari Johason Odour, imesema ilichukuwa muda mrefu kutoa miili kwa family zilizoathirika kutokana na kuharibika kupita kiasi.Soma piaWazee wauliwa pwani ya Kenya kwa tuhuma za kwamba ni wachawiKatika haya  mwanahabari Diana Wanyonyi kutoka pwani ya Kenya  alihudhuria mazishi ya baadhi ya waathiriwa wa mafunzo ya itikadi kali Paul Mackenzie na anasimulia hali ilivyokuwa