Jua Haki Zako

Haki ya watoto chotara shirika la African Futures Lab linataka Ubelgiji kuwatambua

Informações:

Sinopsis

Shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za binadamu la African Futures Lab, lenye makao yake jijini Brussels nchini Ubelgiji, lilizindua ripoti kushinikiza watoto chotara na mama zao kutoka nchini DRC, Rwanda na Burundi, kulipwa fidia, kutambuliwa kuwa raia wa Ubelgiji na kupata haki nyingine za msingi. Wakati wa ukoloni wa nchi ya Ubelgiji kwa nchi hizo za maziwa makuu, wakoloni, wanaume wazungu kutoka nchini Ubelgiji, waliwachukua kwa nguvu wanawake kutoka DRC, Rwanda na Burundi na kuwapeleka Ubelgiji na kuwazalisha, huku wengine wakifanyiwa hivyo wakiwa kwenye nchi zao.Makala haya yameandiliwa na Benson WakoliSoma piaHaki ya mtoto kupata elimu ( Fizi)