Jua Haki Zako

DRC: Waasi wa CODECO wadaiwa kutekeleza mauwaji ya kikabila

Informações:

Sinopsis

Mashariki mwa DRC , vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu vinazidi kushika kasi hasa mauwaji ya raia, vinavyoendelezwa na makundi ya waasi. Makundi haya ni yale  ya ndani na ya kigeni kutoka mataifa jirani ya Uganda "ADF" Sudan kusini "Bororo" na Jamuhuri ya Afrika ya kati "LRA" . Wapiganaji Hao sasa hivi wame fikia hata kiwango cha kushambulia vituo vya afya na kuwazika  raia wakiwa hai.Makala haya yamlika hali  wilayani Djugu mkowani Ituri kaskazini mashariki mwa DRC , ambapo zaidi ya raia  800 wameuawa kikatili na kundi lenye silaha la CODECO katika kipindi cha miaka 6 , kwa mujibu wa mashirika ya kirai mashariki mwa DRC .