Sinopsis
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episodios
-
Baada ya kunusuriwa na programu ya IOM, mhamiaji kutoka nchini Ethiopia asema katu hatorudi Yemen
11/12/2024 Duración: 04minJanga la kibinadamu likizidi kushika kasi nchini Yemen, shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM linaongeza kasi ya mpango wake wa kurejesha wahamiaji nyumbani kwa hiari, VHR. Mradi huu hupatia wahamiaji waliokwama njia salama ya kurejea nyumbani kwao. Kupanuliwa kwa mradi huu kunafuatia idadi ya wahamiaji nchini Yemen kuongezeka na kufikia 6,300 mwezi Oktoba mwaka huu, kwa mujibu wa mfuko wa IOM wa Ufuatiliaji wa wahamiaji.Mwaka huu wa 2024, IOM imeshafanya safari 30 za ndege kupitia mradi huo wa VHR ikiwemo ya tarehe 5 mwezi huu waDesemba ambapo wahamiaji 175 wa Ethiopia walirejeshwa Yemen kutoka uwanja wa ndege wa Aden. Makala hii inafuatilia miongoni mwa wahamiaji hao yaliyowasibu hadi kukubali kurejea nyumbani kwa hiari. Msimulizi wako ni Assumpta Massoi.
-
UNICEF nchini Rwanda kwa kushirikiana na UNICEF Switzerland na Liechtenstein wafanikisha ‘kinesitherapy’ kwa watoto
11/12/2024 Duración: 01minNchini Rwanda Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF kwa msaada wa UNICEF Switzerland na Liechtenstein wamesaidia tiba kwa njia ya mazoezi kuponya watoto wenye ulemavu wa viungo. Selina Jerobon anasimulia akiangazia mtoto mmoja, Joshua.
-
11 DESEMBA 2024
11/12/2024 Duración: 09minHii leo jaridani tunaangazia ripoti ya WHO inayohusu malaria, na juhudi za UNICEF na wadau wake nchini Rwanda za kusaidia watoto waliozaliwa na ulemavu kuweza kutembea. Makala tunakupeleka nchini Yemen na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Takwimu mpya zilizotolewa leo na ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO, zinaonyesha kuwa ingawa takriban wagonjwa bilioni 2.2 wa malaria na vifo milioni 12.7 vya ugonjwa huo vimeepukwa tangu mwaka 2000 bado ugonjwa huo unaendelea kuwa tishio kubwa la kimataifa la afya hususan katika Kanda ya Afrika ya WHO na hivyo juhudi zaidi zahitajika kuutokomeza.Nchini Rwanda Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF kwa msaada wa UNICEF Uswisi na Liechtenstein wamesaidia tiba kwa njia ya mazoezi kuponya watoto wenye ulemavu wa viungo. Selina Jerobon anasimulia akiangazia mtoto mmoja, Joshua.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Yemen kusikia yaliyojiri baada ya ndoto za vijana kuelekea Saudi Arabia kuishia Yemen.Na mashinani mashinani hivi majuzi d
-
WHO: Ingawa vifo milioni 12.7 vya malaria vimeepukwa juhudi zaidi zahitajika kutokomeza gonjwa hilo
11/12/2024 Duración: 01minTakwimu mpya zilizotolewa leo na ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO zinaonyesha kuwa ingawa takriban wagonjwa bilioni 2.2 wa malaria na vifo milioni 12.7 vya ugonjwa huo vimeepukwa tangu mwaka 2000 bado ugonjwa huo unaendelea kuwa tishio kubwa la kimataifa la afya hususan katika Kanda ya Afrika ya WHO. Taarifa ya Flora Nducha inafafanua zaidi.
-
UNFPA: Elimu ndio ufunguo wa kutokomeza FGM Kenya
10/12/2024 Duración: 05minLeo ikiwa ni siku ya kimataifa ya haki za binadamu tunaelekea Kenya kuangazia moja ya ukiukwaji Mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya wanawake, jinamizi la ukeketaji na jitihada zinazochukuliwa na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa ya idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA kutokomeza janga hilo. Mwandishi wetu wa Nairobi Thelma Mwadzaya amefuatilia kuhusu suala hilo na kwa undani zaidi ungana naye ..
-
10 DESEMBA 2024
10/12/2024 Duración: 09minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na tunaelekea nchini Kenya kuangazia moja ya ukiukwaji Mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya wanawake, jinamizi la ukeketaji na jitihada zinazochukuliwa na UNFPA na wadau mbalimbali. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani inayotupeleka nchini Namibia.Baada ya serikali ya Bashar Al-Assad kupinduliwa na kuibuka kwa taarifa za baadhi ya nchi duniani kuanza kusitisha mchakato wa kushughulikia maombi ya Wasyria waliokuwa wameomba hifadhi kuokoa usalama wa maisha yao pindi hali ilipokuwa tete nchini mwao, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) linaendelea kutoa wito kwa mataifa yote kufungua milango, kuwapa hifadhi na ulinzi raia wa Syria wanaotafuta usalama. UNHCR imeahidi pia mara tu hali ya Syria itakapokuwa wazi zaidi, itatoa mwongozo kuhusu mahitaji ya ulinzi kwa Wasyria walioko hatarini.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limekaribisha mchango wa dola za Marekani milioni 22 kutoka shirika la Korea Kusini la Ushir
-
WHO na UNICEF wafikisha chanjo ya polio kwenye maeneo yasiyofikika ya West Pokot Kenya
09/12/2024 Duración: 02minShirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa ushirikiano na serikali ya kenya na wadau wengine wa afya hivi karibuni wamezindua kampeni ya chanjo ya polio katika jamii ya wafugaji na wakulima ya kaunti ya West Pokot Mashariki mwa Kenya ambako mara nyingi ni vigumu kufikiwa. Flora Nducha amefuatilia kampeni hiyo na kutuandalia taarifa ifuatayo..
-
UN yaahidi kusaidia Wasyria kuiboresha nchi yao
09/12/2024 Duración: 01minKufuatia jana Wananchi wa Syria kutwaa madaraka kutoka kwa uongozi uliowatawala kwa mabavu kwa zaidi ya miongo mitano, viongozi wa Umoja wa Mataifa wameendelea kutoa wito wa kuhakikisha mabadiliko haya yanakuwa fursa ya mustakabali bora kwa kuzingatia haki za binadamu, uhuru na haki kisheria. Taarifa iliyoandaliwa na Anold Kayanda inaeleza zaidi.
-
Simfahamu baba yangu, natamani nimfahamu kwani nakosa upendo wake
09/12/2024 Duración: 03minWafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanazuiwa kutumia chakula, fedha au vitu vingine kwa ajili ya kushawishi ngono kutoka kwa mtu mwingine. Operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa zinachukua hatua zaidi kuepusha ukosefu huo wa maadili , lakini bado visa hivyo vinaendelea kutokea. Katika baadhi ya matukio, watoto waliozaliwa kupitia uhusiano wa aiana hiyo wanasalia nyuma kwenye mazingira ya mizozo ambako baada ya baba zao kumaliza kuhudimia, huondoka na kubaki bila baba. Makala hii ya leo inamulika kisa kimoja cha mama na mtoto ambao wamesalia baada ya mlinda amani aliyempatia ujauzito mama husika kuondoka na kurejea nchini mwake. Msimulizi wako ni George Musubao
-
09 DESEMBA 2024
09/12/2024 Duración: 09minHii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Syria, na kampeni ya chanjo ya polio huko Pokot nchini Kenya. Makala tunasalia huko huko DRC na mashinani tnakwenda nchini Msumbiji, kulikoni?Kufuatia jana Wananchi wa Syria kutwaa madaraka kutoka kwa uongozi uliowatawala kwa mabavu kwa zaidi ya miongo mitano, viongozi wa Umoja wa Mataifa wameendelea kutoa wito wa kuhakikisha mabadiliko haya yanakuwa fursa ya mustakabali bora kwa kuzingatia haki za binadamu, uhuru na haki kisheria.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa ushirikiano na serikali ya kenya na wadau wengine wa afya hivi karibuni wamezindua kampeni ya chanjo ya polio katika jamii ya wafugaji na wakulima ya kaunti ya West Pokot Mashariki mwa Kenya ambako mara nyingi ni vigumu kufikiwa.Makala tunakwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikiliza mama ambaye alipatiwa ujauzito na mlinda amani wa Umoja wa Mataifa na kisha kujifungua mtoto ambaye anasimulia kadhia ya kutomf
-
Asante WFP kwa kusambaza dawa za kuua magugu mmebadii maisha yangu: Mkulima Catherine Wanjala
06/12/2024 Duración: 03minMradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP wa kusambaza dawa ya bioherbicide ya kuuwa magugu kwenye mashamba ya mtama na mahindi kwa wakulima wa Kakamega magharibi mwa Kenya umekuwa mkombozi mkubwa kwa wakulima kama Catherine Wanjala ambaye magugu hayo yalimuharibia mazao na hata kuilazimisha familia yale kulala njaa wakati mwingine kwa kukosa chakula. Kwaa ufafanuzi zaidi ungana na Flora Nducha katika makala hii.
-
Miaka 15 ya Mkataba wa Kampala kuhusu wakimbizi wa ndani au IDPs, wito watolewa kwa nchi kuidhinisha na kutekeleza
06/12/2024 Duración: 02minKatika kuadhimisha miaka 15 tangu kupitishwa kwa Mkataba wa Kampala wa Ulinzi na Usaidizi wa Wakimbizi wa Ndani barani Afrika chini Muungano wa Afrika, Kamishna Mkuu Msaidizi wa Ulinzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, Ruven Menikdiwela na Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za Wakimbizi wa ndani Paula Gaviria Betancur wametoa kauli ya pamoja ya kupongeza Muungano wa Afrika kwa maono haya ya mbali na pia kuzisihi nchi zote barani Afrika kuutekeleza mkataba huo muhimu. Selina Jerobon na maelezo zaidi.
-
06 DESEMBA 2024
06/12/2024 Duración: 09minHii leo jaridani tunaangazia Mkataba wa Kampala wa Ulinzi na Usaidizi wa Wakimbizi wa Ndani barani Afrika, na siku ya kimataifa ya kujitolea inayotupeleka nchini DRC. Makala tunakwenda nchini Kenya na mashinani nchini Zambia, kulikoni?Katika kuadhimisha miaka 15 tangu kupitishwa kwa Mkataba wa Kampala wa Ulinzi na Usaidizi wa Wakimbizi wa Ndani barani Afrika chini Muungano wa Afrika, Kamishna Mkuu Msaidizi wa Ulinzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, Ruven Menikdiwela NA Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za Wakimbizi wa ndani Paula Gaviria Betancur wametoa kauli ya pamoja ya kupongeza Muungano wa Afrika kwa maono haya ya mbali na pia kuzisihi nchi zote barani Afrika kuutekeleza mkataba huo muhimu.Dunia ikiwa imeadhimisha siku ya kimataifa ya kujitolea kwa ajili ya amani na maendeleo, tunakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako mmoja wa wafanyakazi wa kujiolea wa Umoja wa Mataifa anaelezea uzoefu wake na ni kwa nini anajivunia kufanya kazi hiyo.M
-
André Bifuko - Najivunia kupatia wengine ujuzi wangu kwa ajili ya amani na maendeleo
06/12/2024 Duración: 01minDunia ikiwa imeadhimisha siku ya kimataifa ya kujitolea kwa ajili ya amani na maendeleo, tunakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako mmoja wa wafanyakazi wa kujiolea wa Umoja wa Mataifa anaelezea uzoefu wake na ni kwa nini anajivunia kufanya kazi hiyo. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
-
Jifunze Kiswahili: Maana ya maneno “MBUKU NA MSUNUNU”
05/12/2024 Duración: 48sKatika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno “MBUKU NA MSUNUNU.”
-
05 DESEMBA 2024
05/12/2024 Duración: 09minHii leo jaridani mada kwa kina inayotupeleka katika makazi ya wakimbizi ya Kyangwali nchini Uganda kumulika hali ya ukatili dhidi ya wanawake kwa watu hao waliokimbia vita jinsi inavyoshughulikiwa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu, UNFPA leo limezindua ombi lake la kimataifa la mwaka 2025, likitafuta dola bilioni 1.4 ili kutoa huduma za afya ya uzazi zinazookoa maisha na programu muhimu za kuzuia unyanyasaji wa kijinsia kwa zaidi ya wanawake, wasichana na vijana milioni 45 kote duniani katika nchi 57 zilizoathiriwa na majanga.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) leo jijini Geneva, Uswisi limetangaza kutoa idhini ya awali kwa kipimo kinachoitwa Xpert® MTB/RIF Ultra dhidi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB). Kipimo hiki pia kinaweza kupima uwezekano wa kuathiriwa kwa viuavijasumu ambacho kinakidhi viwango vya WHO.Biashara ya kimataifa inatazamiwa kufikia dola trilioni 33 mwaka 2024, kulingana na Taarifa mpya ya B
-
Padre Toussaint Murhula: Fikra za kikoloni zimeiharibu Afrika ni wakati wa kuziondoa
04/12/2024 Duración: 03minMkutano wa mwaka 2024 wa Taaluma kuhusu Afrika leo katika leo umeingia siku ya pili hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Mkutano huo ulioandaliwa na Ofisi ya mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Afrika UNOSAA ni wa siku tatu na umebeba maudhui "Nguvu, Haki, na watu” kwa ajili ya mabadiliko ya Afrika.Na moja ya mabadiliko ni kuondoa fikra za kikoloni tangu kufanyika mkutano wa Berlin ulioligawa mapande bara hilo yapata miaka 140 iliyopita amesema mmoja wa washiriki wa mkutano huo aliezungumza na Flora Nducha wa idhaa hii kuhusu kile wanachojadiliana na anaanza kwa kujitambulisha
-
04 DESEMBA 2024
04/12/2024 Duración: 09minHii leo jaridani tunaangazia uzinduzi wa ombi la ufadhili wa mahitaji ya Kibinadamu (GHO), na umuhimu wa lugha mama katika kukuza haki za binadamu. Makala tunasalia hapa makao makuu ya umoja wa mataifa na mashinani tunakupeleka nchini Senegal, kulikoni?Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ikizindua Ripoti ya Kimataifa ya mahitaji ya Kibinadamu (GHO) kwa mwaka ujao wa 2025 imetangaza ombi la ufadhili kwani takriban watu milioni 305 duniani kote watahitaji msaada wa kibinadamu katika mwaka ujao.Haki si haki iwapo inatolewa kwa lugha ambayo haileweki kwa wahusika, wamejulishwa washiriki wa mkutano wa pili wa wanazuoni unaofanyika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani na pia mtandaoni ukimulika Madaraka, Haki na Binadamu: Utawala wa Sheria na mabadiliko Afrika.Makala tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo mkutano wa mwaka 2024 wa Taaluma kuhusu Afrika leo katika leo umeingia siku ya pili hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.
-
Profesa Ngũgĩ wa Thiong’o: Ajabu hata katiba za Afrika ziko kwa lugha za Ulaya
04/12/2024 Duración: 02minHaki si haki iwapo inatolewa kwa lugha ambayo haileweki kwa wahusika, wamejulishwa washiriki wa mkutano wa pili wa wanazuoni unaofanyika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani na pia mtandaoni ukimulika Madaraka, Haki na Binadamu: Utawala wa Sheria na mabadiliko Afrika. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
-
UN na wadau wazindua ombi la dola bilioni 47 kwa ajili ya mwaka 2025
04/12/2024 Duración: 02minOfisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ikizindua Ripoti ya Kimataifa ya mahitaji ya Kibinadamu (GHO) kwa mwaka ujao wa 2025 imetangaza ombi la ufadhili kwani takriban watu milioni 305 duniani kote watahitaji msaada wa kibinadamu katika mwaka ujao. Selina Jerobon na maelezo zaidi.