Sinopsis
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episodios
-
Rwanda yatangaza mwisho wa mlipuko wa Marburg, WHO yapongeza Rwanda
20/12/2024 Duración: 02minShirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) limeipongeza serikali ya Rwanda kwa kufanikiwa kuudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Maburg. Hii leo Rwanda imetangaza mwisho wa mlipuko wa hivi karibuni wa ugonjwa huo baada ya kutokuwepo maambukizi mapya katika siku 42 na mgonjwa wa mwisho akiwa amepimwa mara mbili bila kukutwa na ugonjwa kama matakwa ya WHO yanavyotaka ili kutangaza kuisha kwa mlipuko wa magonjwa namna hii. Selina Jerobon na maelezo zaidi.
-
20 DESEMBA 2024
20/12/2024 Duración: 10minHii leo jaridani tunaangazia jitihada za kuudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Maburg nchini Rwanda, na juhudi za kuchunguza virusi vya VVU nchini Ghana. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini DRC, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) limeipongeza serikali ya Rwanda kwa kufanikiwa kuudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Maburg. Hii leo Rwanda imetangaza mwisho wa mlipuko wa hivi karibuni wa ugonjwa huo baada ya kutokuwepo maambukizi mapya katika siku 42 na mgonjwa wa mwisho akiwa amepimwa mara mbili bila kukutwa na ugonjwa kama matakwa ya WHO yanavyotaka ili kutangaza kuisha kwa mlipuko wa magonjwa namna hii.Mwaka 2020 Ghana iliripoti kuwa na watu 350,000 wanaioshi na virusi vya Ukimwi na kati yao hao 31,000 walikuwa ni wajawazito. Jambo lililoshtua ni kwamba ni sehemu ndogo mno ya wajawazito hao ndio walipimwa kufahamu iwapo wana VVU au la. Jambo lililofanya serikali kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kuchukua hatua.Makala inatupeleka kwenye ka
-
Kipimo cha GeneXpert chaleta mapinduzi kwenye upimaji wa VVU nchini Ghana
20/12/2024 Duración: 02minMwaka 2020 Ghana iliripoti kuwa na watu 350,000 wanaioshi na virusi vya Ukimwi na kati yao hao 31,000 walikuwa ni wajawazito. Jambo lililoshtua ni kwamba ni sehemu ndogo mno ya wajawazito hao ndio walipimwa kufahamu iwapo wana VVU au la. Jambo lililofanya serikali kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kuchukua hatua. Ripoti ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi.
-
Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa neno Akraba
19/12/2024 Duración: 38sKatika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya neno “AKRABA.”
-
19 DESEMBA 2024
19/12/2024 Duración: 09minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Syria, ambako viongozi wa ngazi mbalimbali za Umoja wa Mataifa wamendelea kusisitiza hitaji la kutanguliza ulinzi wa manusura na uhifadhi wa ushahidi wa uhalifu. Pia tunapata ufafanuzi wa neno na muhtasari wa habari.Karla Quintana kutoka Mexico ameteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres hii leo kuongoza Taasisi Huru ya kuchunguza watu waliotoweshwa nchini Syria, taasisi ambayo imeundwa na Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Juni mwaka jana 2023. Guterres amewaambia waandishi wa habari hii leo kwamba yeye na timu yake lazima waruhusiwe kutekeleza kwa kina jukumu lao, na vile vile mifumo yote ya kimataifa ya kusongesha ulinzi wa haki za binadamu nchini Syria na uwajibikaji wa uhalifu uliotendwa lazima wawe na wanachohitaji ili kutekeleza majukumu yao muhimu.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa na kikao cha ngazi ya mawaziri kuhusu Akili Mnemba, au AI ambapo Katibu Mkuu António Guterres amesema pamoja faida kub
-
FAO Tanzania yatoa mafunzo ya ufugaji wa nyuki kwa wenyeji Tanzania kupitia Mradi wa ACP MEAs 3
18/12/2024 Duración: 02minMradi wa ACP MEAs 3 unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO, na kufadhiliwa na Muungano wa Ulaya, EU umetoa mafunzo ya ufugaji nyuki kwa wakulima nchini Tanzania. Mradi huu unawapa wakulima zana na ujuzi muhimu katika ufugaji nyuki endelevu, na hivyo kuboresha maisha yao huku wakikuza bayoanuwai na uhifadhi wa mazingira. Kwa kuunga mkono jamii za wenyeji, Mradi huu unalenga kukuza ukuaji wa uchumi na kuwawezesha wakulima kulinda wachavushaji, ambao ni muhimu kwa uzalishaji katika kilimo na afya ya mfumo ikolojia. Tupate simulizi zaidi katika makala hii iliyoandaliwa na Flora Nducha kupitia video ya FAO Tanzania.
-
Guterres: Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji tujikumbushe changamoto wanazokumbana nazo
18/12/2024 Duración: 01minIkiwa leo ni siku ya kimataifa ya Uhamiaji, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake mahususi kwa ajili ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji ametoa wito kwa ulimwengu kuitumia siku hii kujikumbusha kwamba pamoja na kwamba tunasherehekea michango ambayo mamilioni ya wahamiaji hutoa kwa jamii leo pia ni siku ya kujikumbusha changamoto ambazo wahamiaji wanaweza kukumbana nazo. Selina Jerobon na maelezo zaidi.
-
18 DESEMBA 2024
18/12/2024 Duración: 09minHii leo jaridani tunaangazia siku ya wahamiaji duniani ikimulika mchango wa wakimbizi na wahamiaji katika ukuaji wa kiuchumi na kukuza jamii zao n aza wenyeji. Tutasikia kutoka mkuu wa IOM, Katibu Mkuu wa UN na wahamiaji Burundi na Chad. Pia tunaangazia ufugaji nyuki Tanzania.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake mahususi kwa ajili ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji ametoa wito kwa ulimwengu kuitumia siku hii kujikumbusha kwamba pamoja na kwamba tunasherehekea michango ambayo mamilioni ya wahamiaji hutoa kwa jamii leo pia ni siku ya kujikumbusha changamoto ambazo wahamiaji wanaweza kukumbana nazo.Nimefurahi sana kwani binti yangu mwenye ulemavu ambaye tulihamia naye makazi ya muda kufuatia kuongezeka kina cha maji ya Ziwa Tanganyika, hapa Burundi sasa amepatiwa stadi za kumwezesha kujikwamua kiuchumi. Ni kauli ya Odette Niyonkuru, raia mhamiaji wa ndani nchini Burundi akizungumzia mustakabali wa binti yake huyo kwenye video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM.Makala i
-
Mafunzo ya IOM kwa msichana mhamiaji mwenye ulemavu, yaleta furaha kwa mama yake
18/12/2024 Duración: 02minNimefurahi sana kwani binti yangu mwenye ulemavu ambaye tulihamia naye makazi ya muda kufuatia kuongezeka kina cha maji ya Ziwa Tanganyika, hapa Burundi sasa amepatiwa stadi za kumwezesha kujikwamua kiuchumi. Ni kauli ya Odette Niyonkuru, raia mhamiaji wa ndani nchini Burundi akizungumzia mustakabali wa binti yake huyo kwenye video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM. Odette anaenelea kueleza manufaa ya uwezeshaji huu kwa bintiye kama anavyofuatilia Assumpta Massoi.
-
17 DESEMBA 2024
17/12/2024 Duración: 10minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika mafanikio katika kuzuia maambukizi mapya ya VVU na juhudi za vijana wakimbizi nchini Uganda kuhakikisha hilo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani inayotupeleka Gaza.Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Geir O. Pedersen bado yuko nchini Syria alikowasili jana Jumapili ikiwa ni wiki moja baada ya wapiganaji wa Hayʼat Tahrir al-Sham (HTS) walioko kwenye orodha ya vikundi vya kigaidi kutwaa mji mkuu Damascus na kusababisha Rais Bashar Al-Assad kukimbia nchi.Mwaka 2024 ukielekea ukingoni, sirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Uganda limetoa rai kwa jumiya ya kimataifa kutolisahau taifa hilo la Afrika Mashariki ambalo ni maskani ya idadi kubwa zaidi ya waomba hifadhi na wakimbizi barani Afrika. Rai hiyo iliyotolewamwishoni mwa wiki inataka ufadhili wa fedha uongezwe ili liweze kuendelea kukirimu watu hao ambao wengi wanakimbia machafuko.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,
-
Harakati za wazazi kuona watoto wao wanasajiliwa nchini mwao baada ya kuzaliwa
16/12/2024 Duración: 04minTarehe 11 mwezi huu wa Desemba, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF lilitoa ripoti yake kuhusu usajili wa vizazi duniani ikionesha maendeleo makubwa katika idadi ya watoto wanaosajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa. Maeneo mengine kama nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara ongezeko ni dogo ikilinganishwa na kwingineko. Ingawa hivyo licha ya changamoto zilizoko kwa nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara katika kutoa huduma hiyo, mafanikio yanaanza kuonekana kama inavyosimulia makala hii iliyoandaliwa na Assumpta Massoi kupitia video ya UNICEF.
-
Mjumbe wa UN aendelea na ziara ya kukutana na wadau nchini Syria
16/12/2024 Duración: 01minMjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Geir O. Pedersen bado yuko nchini Syria alikowasili jana Jumapili ikiwa ni wiki moja baada ya wapiganaji wa Hayʼat Tahrir al-Sham (HTS) walioko kwenye orodha ya vikundi vya kigaidi kutwaa mji mkuu Damascus na kusababisha Rais Bashar Al-Assad kukimbia nchi. Ikiwa ni sehemu ya juhudi za Umoja wa Mataifa kuhakikisha mabadiliko ya utawala nchini Syria yanafanyika kwa amani na kuisaidia Syria kutokuingia kwenye mgogoro zaidi, Bwana Pederson aliyewasili jana Damascus hadi sasa ameshakutana na Kamanda wa Utawala Mpya Ahmed al-Sharaa na Waziri Mkuu wa Serikali ya Muda Mohammed al-Bashir.Taarifa iliyotolewa leo na Ofisi yake inasema Pederson ameeleza muhtasari wa matokeo ya Mkutano wa Kimataifa wa Aqaba kuhusu Syria uliofanyika tarehe 14 ya mwezi huu wa Desemba akisisitiza haja ya kuwepo kwa mpito wa kisiasa unaoaminika na unaoongozwa na kumilikiwa na Wasyria wenyewe kama kanuni za azimio 2254 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (2015) zilivyopendekeza.
-
16 DESEMBA 2024
16/12/2024 Duración: 09minHii leo jaridani tunaangazia serikali ya mpito nchini Syria na wakimbizi na wahamiaji wanaosaka hifadhi nchini Uganda. Makala tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Geir O. Pedersen bado yuko nchini Syria alikowasili jana Jumapili ikiwa ni wiki moja baada ya wapiganaji wa Hayʼat Tahrir al-Sham (HTS) walioko kwenye orodha ya vikundi vya kigaidi kutwaa mji mkuu Damascus na kusababisha Rais Bashar Al-Assad kukimbia nchi.Mwaka 2024 ukielekea ukingoni, sirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Uganda limetoa rai kwa jumiya ya kimataifa kutolisahau taifa hilo la Afrika Mashariki ambalo ni maskani ya idadi kubwa zaidi ya waomba hifadhi na wakimbizi barani Afrika. Rai hiyo iliyotolewamwishoni mwa wiki inataka ufadhili wa fedha uongezwe ili liweze kuendelea kukirimu watu hao ambao wengi wanakimbia machafuko.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Et
-
UNHCR: Chonde chonde jumuiya ya Kimataifa tuishike mkono Uganda kwa faida ya waomba hifadhi na wakimbizi
16/12/2024 Duración: 02minMwaka 2024 ukielekea ukingoni, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Uganda limetoa rai kwa jumuiya ya kimataifa kutolisahau taifa hilo la Afrika Mashariki ambalo ni maskani ya idadi kubwa zaidi ya waomba hifadhi na wakimbizi barani Afrika. Rai hiyo iliyotolewa mwishoni mwa wiki inataka ufadhili wa fedha uongezwe ili liweze kuendelea kukirimu watu hao ambao wengi wanakimbia machafuko. Huyo ni Moulid Hujale afisa wa UNHCR nchini Uganda akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kushikamana na Uganda akiwa kwenye makazi makubwa ya wakimbizi ya Kiryandongo Magharibi mwa nchi hiyo. Anasema kuna mambo matatu muhimu ambayo dunia inapaswa kufahamu kuhusu Uganda na wakimbizi.“Mosi Uganda inahifadhi idadi kubwa zaidi ya wakimbizi na waomba hifadhi Afrika ikiwa na zaidi ya watu milioni 1.7 wengi wao wakitoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na Sudan Kusini.”Zaidi ya hapo ukarimu wa Uganda anasema hauna kipimo“Pili, Uganda ina sera ya kufugua mlango kwa wakimbizi na pia kwa miong
-
Sasa tunalima mboga shuleni na nyumbani - Wanafunzi Buhigwe Tanzania
13/12/2024 Duración: 03minKupitia mradi wa Pamoja wa Kigoma, KJP, awamu ya Pili, Shule ya Msingi Buhigwe, iliyoko wilayani Buhigwe, mkoa wa Kigoma, ilipatiwa mafunzo kupitia Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), likishirikiana na asasi isiyo ya kiserikali RECODA. Mafunzo haya yalilenga mbinu bora za kilimo ambapo wanafunzi waliweza kuanzisha bustani za mboga kupitia somo la Elimu ya Kujitegemea. Mradi umeanza kutekelezwa na matunda yanaanza kuonekana kama asimuliavyo Assumpta Massoi kwenye makala hii.
-
UNFPA yasambaza huduma muhimu ya ukunga kwa wakimbizi wa Sudan nchini Chad
13/12/2024 Duración: 01minKutokana na idadi kubwa ya wakimbizi wanaoingia Chad wakitoka Sudan kuwa ni wanawake na watoto, Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi, UNFPA limeimarisha huduma za afya ya wanawake na watoto kama anavyosimulia Selina Jerobon.
-
13 DESEMBA 2024
13/12/2024 Duración: 09minHii leo jaridani tunaangazia hali nchini Syria, na msaada wa kibinadamu kw awakimbizi nchini Chad. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, kulikoni?Ofisi ya mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria (OSE) imesema wakati huu ikifuatilia kwa karibu hali na maendeleo nchini Syria ni muhimu kuhakikisha kwamba Wasyria wanashika usukani wa mustakbali wao na kwamba kuna ujumbe wa pamoja na mshikamono kuhusu hilo kutoka kwenye jumuiya ya kimataifa.Kutokana na idadi kubwa ya wakimbizi wanaoingia Chad wakitoka Sudan kuwa ni wanawake na watoto, Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi, UNFPA limeimarisha huduma za afya ya wanawake na watoto.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Tanzania kusikia jinsi wanafunzi wananufaika na mradi wa Umoja wa Mataifa shuleni na majumbani.Na mashinani fursa ni yake Aline kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC ambaye ni mnufaika wa mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula
-
UN: Lazima kuhakikisha Wasyria wanashika usukani wa mustakbali wao
13/12/2024 Duración: 01minOfisi ya mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria (OSE) imesema wakati huu ikifuatilia kwa karibu hali na maendeleo nchini Syria ni muhimu kuhakikisha kwamba Wasyria wanashika usukani wa mustakbali wao na kwamba kuna ujumbe wa pamoja na mshikamono kuhusu hilo kutoka kwenye jumuiya ya kimataifa. Flora Nducha na taarifa zaidi.
-
Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi maana ya neno MIDABWADA
12/12/2024 Duración: 28sKatika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno MIDABWADA”
-
12 DESEMBA 2024
12/12/2024 Duración: 10minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa ikiangazia wanawake na wasichana mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ambapo ukatili wa kingono ni jinamizi linalowakumba kila uchao kutokana na mapigano yanayoendelea kwenye eneo hilo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno MIDABWADA.Leo si siku ya kimataifa ya huduma za afya kwa wote mwaka huu ikibeba mudhui “Huduma za afya kwa wote ni jukumu la serikali” yakisisitiza kwamba Uwekezaji katika huduma za afya kwa wote UHC, unaimarisha usawa na uwiano wa kijamii na pia unanufaisha uchumi wa taifa kwa kuboresha afya na ustawi, kuongeza ushiriki wa wafanyikazi na tija, na kujenga mnepo kwa watu, familia na jamii.Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syri Geir O. Pedersen leo amesema “Picha kutoka kwenye magereza ya Sednaya na vituo vingine vya kizuizini nchini Syria vinadhihirisha unyama na ukatili usiofikirika ambao Wasyria wamevumilia na umekuwa ukiripotiwa kwa miaka mingi.”Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres yuko z