Sinopsis
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episodios
-
Dayspring Foundation nchini Tanzania yatekeleza kivitendo dhana ya UN ya michezo kwa maendeleo
07/04/2025 Duración: 04minSiku ya kimataifa ya Michezo kwa ajili ya Maendeleo na Amani imeadhimishwa tarehe 6 mwezi huu wa Aprili maudhui yakiwa Ujumuishaji wa kijamii, hususan makundi ya pembezoni. Umoja wa Mataifa kupitia wavuti wake unasema kuwa siku hii inatambuliwa kutokana na nafasi ya michezo katika kuleta mabadiliko chanya, kuondoa vikwazo na kuvuka mipaka. Na usuli wa maudhui ya mwaka huu ni kwamba fikra potofu kwenye jamii zimesababisha baadhi ya watu kutokana na jinsia yao, umri, au rangi wanashindwa kushiriki kwenye michezo ambayo kwa njia moja au nyingine hutokomeza umaskini kwa kuwezesha washiriki kujipatia kipato. Nchini Tanzania shirika la kiraia la Dayspring Foundation limetambua nafasi ya michezo na limeanza kuchukua hatua. Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Rosemary Mwaipopo ambaye anaanza kwa kuelezea ni kwa nini waliamua kujikita katika kusaka vipaji.
-
Kwibuka2025: Katibu Mkuu UN ahimiza mshikamano wa kimataifa dhidi ya chuki
07/04/2025 Duración: 02minDunia inapokumbuka miaka 31 tangu mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma ujumbe mzito wa maombolezo na onyo, akitaka mshikamano wa kimataifa kupambana na ongezeko la chuki, mgawanyiko, na misimamo mikali kupitia mifumo ya kidijitali. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
-
07 APRILI 2025
07/04/2025 Duración: 11minHii leo jaridani tunaangazia makumbusho ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, na Siku ya Afya Duniani. Makala inamulika nafasi ya michezo katika kusongesha amani na maendeleo, na mashinani tunakwenda nchini Kenya, kulikoni?Dunia inapokumbuka miaka 31 tangu mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma ujumbe mzito wa maombolezo na onyo, akitaka mshikamano wa kimataifa kupambana na ongezeko la chuki, mgawanyiko, na misimamo mikali kupitia mifumo ya kidijitali.Leo ni Siku ya Afya Duniani ambayo mwaka huu inangazia suala muhimu kwa afya ya dunia, changamoto maalum wanazokumbana nazo wanawake na wasichana lakini pia vifo vya watoto wachanga, na ili kuhakikisha changamoto hizo zinashughulikiwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO limezindua kampeni ya mwaka mzima ya “Mwanzo wenye afya ni mustakbali wenye matumaini”..Makala inamulika nafasi ya michezo katika kusongesha amani na maendeleo, ambapo Assump
-
Hatua za haraka zinahitajika sasa kuzuia vifo na kulinda afya ya wanawake na wasichana: UN
07/04/2025 Duración: 02minLeo ni Siku ya Afya Duniani ambayo mwaka huu inangazia suala muhimu kwa afya ya dunia, changamoto maalum wanazokumbana nazo wanawake na wasichana lakini pia vifo vya watoto wachanga, na ili kuhakikisha changamoto hizo zinashughulikiwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO limezindua kampeni ya mwaka mzima ya “Mwanzo wenye afya ni mustakbali wenye matumaini”. Flora Nducha anafafanua zaidi.
-
Uongozi bora na matumizi bora ya rasilimali vitaikomboa Afrika kimaendeleo: Vijana Kenya
04/04/2025 Duración: 03minMajadiliano ya siku mbili yanayofanyika kila mwaka ya será kuhusu maendeleo endelevu. Majadiliano hayo yanayokunja jamvi leo jijini Nairobi Kenya yameandaliwa na Club De Madrid na mwaka huu yakijikita na ufadhili wa maendeleo na kuwaleta pamoja wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wastaafu w anchi na serikali, wadau wa maendeleo na vijana. Stella Vuzo kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi amepata fursa ya kuzungumza na baadhi ya vijana wanaoshiriki mkutano huo wa club de Madrid je wanasemaje? Ungana nao katika makala hii
-
Umoja wa Mataifa kuendelea kuisaidia Somalia kuonda mabomu ya kutegwa ardhini
04/04/2025 Duración: 01minIkiwa leo ni Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini na Msaada wa Hatua Dhidi ya Mabomu hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akisisitiza mataifa duniani kote kuheshimu mikataba ya kimataifa dhidi ya vilipuzi na silaha nyingine, Umoja wa Mataifa leo umethibitisha tena dhamira yake ya kusaidia Somalia katika mapambano dhidi ya hatari za vilipuzi kwa ajili ya mustakabali salama kwa Wasomali wote. Anold Kayanda na taarifa zaidi.
-
04 APRILI 2025
04/04/2025 Duración: 09minHii leo jaridani tunaangazia Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini. Makala inamulika harakati za kusongesha malengo ya maendeleo endelevu ikitupeleka nchini Kenya na mashinani tunasalia huko huko nchini Kenya, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini na Msaada wa Hatua Dhidi ya Mabomu hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akisisitiza nchi kuheshimu mikataba ya kimataifa dhidi ya vilipuzi na silaha nyingine, Umoja wa Mataifa leo umethibitisha tena dhamira yake ya kusaidia Somalia katika mapambano dhidi ya hatari za vilipuzi kwa ajili ya mustakabali salama kwa Wasomali wote.Mwaka huu wa 2025, Siku ya Kimataifa ya Uhamasishaji Kuhusu Mabomu ya Ardhi na Usaidizi kwa Hatua Dhidi ya Mabomu inaadhimishwa chini ya kaulimbiu “Mustakabali Salama Unaanzia Hapa.” Umoja wa Mataifa inasisitiza umuhimu wa kufadhili miradi midogo yenye athari za haraka kusaidia watu wenye ulemavu wa viungo waliathirika katika mizozo. Juhudi hizi zinaimarisha u
-
Uteguaji mabomu ya ardhini ni suala la amani na kiutu - UNMAS
04/04/2025 Duración: 02minIkiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini, kauli mbiu ikiwa Mustakabali salama unaanzia hapa, Umoja wa Mataifa unasisitiza umuhimu wa kufadhili miradi midogo yenye matokeo chanya na ya haraka ili kusaidia sio tu watu wanaopata ulemavu wa viungo kutokana na madhara ya mabomu hayo bali pia kuwezesha watu kurejea kwenye maisha yao ya kawaida Sharon Jebichii anamulika Lebanon na Libya.
-
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "MHARUMA.”
03/04/2025 Duración: 31sKatika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MHARUMA.”
-
03 APRILI 2025
03/04/2025 Duración: 11minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha kwenye mkutano wa hivi majuzi wa CSW69 kufuatilia harakati za Mfuko wa CRDB za kujengea uwezo na kuinua wanawake nchini Tanzania. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno “MHARUMA.”Mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wa misaada ya kibinadamu leo wamesema wanaendelea kuwasaidia watu wa Muyanmar na mahitaji ya msingi baada ya tetemeko kubwa la ardhi la Ijuma iliyopita ambapo idadi ya waliopoteza maisha sasa ni zaidi ya 2,800, maelfu wamejerihiwa na mamia bado hawajulikani wako.Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Türk, amesema leo kwamba ameshtushwa na ripoti za mauaji ya raia bila kufuata utaratibu wa kisheria yaliyoenea mjini Khartoum baada ya kurejeshwa kwa mji huo chini ya udhibiti wa Jeshi la Sudan (SAF) tarehe 26 Machi.Na majadiliano ya siku mbili ya kila mwaka ya será kuhusu maendeleo endelevu yaliyoandaliwa na Club De Madrid yameanza leo Nairobi Kenya mwaka huu yakijikita na ufadhili wa maendeleo. shudu
-
UN na wadau wasadie chanzo cha usonji kifahamike - Lukiza Foundation
02/04/2025 Duración: 04minHii leo dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu usonji, Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imezungumza na Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lukiza Foundation nchini Tanzania inayoelimisha umma kuhusu usonji. Usonji ni hali inayompata mtoto au utofauti au changamoto katika mfumo wake wa ufahamu na ubongo na kusababisha changamoto za kimawasiliano, tabia na kudhibiti hisia mwili. Hoja kubwa ni kwamba hadi sasa sababu ya hali hiyo kumpata mtoto haijajulikana na ndipo taasisi hiyo inachagiza Umoja wa Mataifa na wadau washikamane katika tafiti kujua chanjo kama njia mojawapo ya kudhibiti au kutibu ugonjwa huo. Basi kwa kina kufahamu harakati za taasisi hiyo nchini Tanzania, nampisha Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.
-
Ujumbe wa Katibu Mkuu UN Siku ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma Kuhusu Usonji
02/04/2025 Duración: 01minKatika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma kuhusu Usonji (Autism) mwaka huu wa 2025, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesisitiza umuhimu wa ujumuishaji na usawa kwa watu wenye changamoto hiyo akitambua mafanikio yao pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo duniani kote. Anold Kayanda anaeleza zaidi.
-
02 APRILI 2025
02/04/2025 Duración: 09minHii leo jaridani tunaangazia Siku ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma kuhusu Usonji, na wakimbizi wa ndani nchini DRC. Makala inatupeleka nchini Tanzania kwa mada hiyo hiyo ya elimu kuhusu usonji, na mashinani tunakwenda Gaza.Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma kuhusu Usonji (Autism) mwaka huu wa 2025, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesisitiza umuhimu wa ujumuishaji na usawa kwa watu wenye changamoto hiyo akitambua mafanikio yao pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo duniani kote.Jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Thérèse Kavira, mwanamke shupavu aliyelazimika kukimbilia mji wa Beni baada ya waasi kuvamia kijiji chake sasa ameona nusu kwenye maisha yake kufuatia mafunzo ya kuoka mikate yaliyotolewa na ofisi ya Utafiti na Usaidizi kwa Mahusiano ya Kimataifa nchini humo pamoja na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani DRC, MONUSCO na sasa anajikimu kimaisha.Makala leo kama tulivyokujulisha ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umm
-
Stadi za kuoka mikate zaleta furaha kwa mkimbizi Thérèse huko Beni nchini DRC
02/04/2025 Duración: 01minJimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Thérèse Kavira, mwanamke shupavu aliyelazimika kukimbilia mji wa Beni baada ya waasi kuvamia kijiji chake sasa ameona nusu kwenye maisha yake kufuatia mafunzo ya kuoka mikate yaliyotolewa na ofisi ya Utafiti na Usaidizi kwa Mahusiano ya Kimataifa nchini humo pamoja na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani DRC, MONUSCO na sasa anajikimu kimaisha. Sharon jebichii na taarifa zaidi.
-
Tanzania: UNICEF na Ubalozi wa Uholanzi wamesaidia kupunguza magonjwa Kilolo
28/03/2025 Duración: 01min -
-
28 MACHI 2025
28/03/2025 Duración: 09minUmoja wa Mataifa watuma salamu za rambirambi kufuatia tetemeko barani Asia.UNICEF na Ubalozi wa Uholanzi wamesaidia kupunguza magonjwa Kilolo, Tanzania.Makala ni kuhusu Siku ya Kimataifa ya Kutozalisha Taka.Mashinani tunamulika ubunifu wa Janet Chemitei wa Tengeneza Cafe katika urejelezaji nguo nchini Kenya.
-
METHALI: NDOTO NJEMA HAIHADITHIWI
27/03/2025 Duración: 01minKaribu kujifunza Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye Kitivo cha Tafsiri na Ukalimani na anafafanua methali Ndoto njema haihadithiwi.
-
27 MACHI 2025
27/03/2025 Duración: 11minKaribu kusikiliza jarida la Umoja wa Mataifa ambapo hii leo tunaendelea na kuwasikia wadau waliohudhuria mkutano uliomalizika wiki iliyopita wa Kamisheni ya hali ya wanawake CSW69 unaotathmini Azimio la Beijing na Mpango wa Utekelezaji vilivyopitishwa mwaka 1995 katika mkutano wa 4 wa kimataifa wa wanawake huko Beijing China. Pia utapata fursa ya kusikiliza muhtasari wa habari na kujifunza kiswahili ambapo leo utapata ufafanuzi wa methali "NDOTO NJEMA HAIHADITHIWI"
-
Chad: Wanakikundi watumia faida ya biashara yao kuanzisha shule
26/03/2025 Duración: 03minNchini Chad, wanawake wanakikundi cha kutengeneza sabuni na mafuta ya kupata mwilini wameamua kuchukua hatua ili umamuma wa kutokujua kusoma na kuandika ambao umewakumba wao, usiwakumbe pia watoto wao wa kike. Wanakikundi hao wa APROFiCA wanaopata ufadhili kutoka Benki ya Dunia wameona ni vema kuchukua hatua hiyo ili kufanikisha lengo namba 4 la Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs la Umoja wa Mataifa kuhusu elimu, kwani elimu ni mkombozi kwa binadamu. Je wamefanya nini? Assumpta Massoi anafafanua kupitia video ya Benki ya Dunia.