Sinopsis
Listen to interviews, features and community stories from the SBS Radio Swahili program, including news from Australia and around the world. - Sikiza mahojiano, makala na hadithi za jumuiya kutoka Idhaa ya Kiswahili ya SBS Radio, ikijumuisha taarifa za habari kutoka Australia na ulimwenguni.
Episodios
-
Afya ya akili:kupata usaidizi kama mhamiaji
10/11/2025 Duración: 08minWahamiaji wengi wanakumbana na matatizo tofauti wanapojaribu kupata msaada wa afya ya akili. Umoja wa Mataifa unasema kwamba upatikanaji wa huduma za afya ya akili ni haki ya msingi kwa kila mtu , ikiwemo wahamiaji na wakimbizi. Umoja wa Mataifa unasisitiza kwamba wahamiaji mara nyingi wanakabiliwa na changamoto nyingi kama vile msongo wa mawazo, huzuni, kiwewe na ata upweke kutokana na mazingira mapya. Mtaalamu wa Afya ya Akili Terry Kiguru anatueleza jinsi ya kupata msaada huo na kwanini.
-
Jamii ya Sudan walio Australia waendelea kuwa na wasiwasi
10/11/2025 Duración: 08minJamii ya watu wa Sudan walio nchini Australia wana wasiwasi mkubwa ,wakisubiri habari kutoka kwa familia zao walionaswa katika jiji la Al-Fasher baada ya mlipuko wa ghasia. Jiji hilo lilitekwa na Rapid Support Forces wiki mbili iliyopita, na wataalamu wanaamini kwamba maelfu huenda wameuawa katika mauaji ya kutisha. Kwa kuwa huduma za intaneti na simu zimekatwa, wanaoishi nje ya nchi wanalazimika kukaa na kusubiri ili kujua kama wapendwa wao bado wako hai.
-
Umaskini wa nishati
10/11/2025 Duración: 07minMaelfu ya kaya za Wenyeji kaskazini mwa Australia wanaishi na mfumo wa kulipa kabla wa umeme, ambapo kukatwa kunaweza kutokea wakati wowote. Ripoti mpya sasa imeonya kwamba bila ulinzi wa kutosha, mfumo huu unaweza kuwa hatari katika joto kali.
-
Hali ya hewa inawaathiri pinguini
08/11/2025 Duración: 05minTimu ya kimataifa ya wanasayansi imeonya kuwa pIngwini wanaweza kuwa katika hatari kutokana na madhara ya hali mbaya ya hewa. Utafiti mpya unapendekeza kwamba si tukio moja kama vile joto kali inayosababisha hatari kubwa zaidi, bali ni athari zake zilizoungana pamoja katika ardhi na baharini.
-
Mzio wa karanga kwa watoto upata mwelekeo mpya
04/11/2025 Duración: 07minMiaka kumi baada ya utafiti muhimu kudhibitisha kwamba kuwalisha watoto wachanga bidhaa za karanga inaweza kuendeleza mzio hatari, utafiti mpya umebaini kuwa kuna uwezekano wa kuepuka kuendeleza mizio ya chakula.
-
Serikali kudhibitisha umuhimu wa wahamiaji kwenye uchumi
04/11/2025 Duración: 05minWaziri wa Mambo ya Ndani, Tony Burke, anasema kwamba serikali inafanya kazi juu ya uwezekano wa kutambua ujuzi wa nje ya nchi. Anasema hii itasaidia kuokoa muda na pesa kwa wahamiaji wenye ujuzi wanaotafuta kuhamia Australia. Katika hotuba yake kwa Klabu ya Waandishi wa Habari huko Canberra, Bw. Burke pia ametangaza mabadiliko kwenye akaunti za benki zisizotumika ili kukabiliana na utakatishaji wa fedha.
-
Understanding treaty in Australia: What First Nations people want you to know - Mkataba wa amani: Una maana gani na Una manufaa gani
04/11/2025 Duración: 05minAustralia is home to the world’s oldest living cultures, yet remains one of the few countries without a national treaty recognising its First Peoples. This means there has never been a broad agreement about sharing the land, resources, or decision-making power - a gap many see as unfinished business. Find out what treaty really means — how it differs from land rights and native title, and why it matters. - Waingereza walipowasili Australia walitangaza ardhi kuwa ‘terra nullius’ kumaanisha ardhi isiyomilikiwa na yeyote. Hawakuona haja ya kuzungumza na mataifa ya waaboriginals na kwa hivyo wenyeji wa Australia wanasema kwamba hii ni biashara ambayo haijakamilika.
-
Taarifa ya Habari 26 Septemba 2025
26/09/2025 Duración: 14minWaziri wa Mambo ya Nje Penny Wong amesema Australia ina simama kidete juu ya tamaduni nyingi, baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kukosoa uhamiaji katika hotuba yake kwa kikao cha mkutano wa Umoja wa Mataifa.
-
Taarifa ya Habari 23 Septemba 2025
23/09/2025 Duración: 17minWaziri Mkuu amesema ombi la utaifa wa Palestina ni fursa ya amani, katika hotuba yake kuhusu soluhu ya nchi mbili, alipo hudhuria kikao cha Umoja wa Mataifa hii leo Jumanne 23 Septemba 2025.
-
Serikali ya shirikisho yazungumza kwa ukali baada ya kupotea kwa huduma ya simu ya dharura ya Optus
23/09/2025 Duración: 09minWaziri wa Shirikisho wa Mawasiliano amesema Optus inastahili tarajia adhabu kubwa, kufuatia kupotea kwa huduma ya namba ya dharura ya 000, hali ambayo ime husishwa na vifo kadhaa.
-
Kamerhe chini ya shinikizo kuondolewa kama spika wa bunge la DRC
22/09/2025 Duración: 06minTaratibu zinazolenga kumfuta kazi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Vital Kamerhe zinaendelea huku kukishuhudiwa hali ya mfarakano kati ya rais Félix Tshisekedi na mshirika wake huyo wa zamani.
-
Taarifa ya Habari 19 Septemba 2025
19/09/2025 Duración: 14minKampuni ya pili kwa ukubwa ya madini imetangaza inapunguza ajira. Anglo American Australia imesema ita angaza kupunguza idadi ya wafanyakazi Queensland, na takriban wafanyakazi 200 wata athirika.
-
Raia wapya wa Australia wakaribishwa katika sherehe katika Siku ya Uraia ya Australia
19/09/2025 Duración: 11minMaelfu ya watu wanasherehekea kuwa raia wapya wa Australia, katika sherehe zilizo andaliwa na halamshauri za jiji kote nchini kwa siku ya Uraia wa Australia.
-
SBS Learn Eng Ep 93 Namna ya kujigamba kuhusu gari lako katika Kiingereza
19/09/2025 Duración: 16minJe, unajua jinsi ya kujigamba kuhusu gari lako?
-
Taarifa ya Habari 16 Septemba 2025
16/09/2025 Duración: 15minNaibu Waziri Mkuu Richard Marles amekana madai kuwa uwekezaji wa $12 bilioni iliyo tangazwa juzi ime undwa ili kutuliza maombi ya Marekani kwa Australia kuongeza matumizi yake katika ulinzi.
-
SBS Learn Eng Ep 95 Anga la usiku
16/09/2025 Duración: 13minJe, unajua jinsi ya kuelezea kuhusu anga la usiku?
-
Kitu chakufanya unapo kutana na wanyamapori kwenye mali yako
15/09/2025 Duración: 12minPopote ulipo nchini Australia, kutoka jiji kuu lenye shughuli nyingi, hadi katika viunga vya mji, katika mji wa kikanda au kijijini, kuna uwezekano unaweza kutana na aina mbali mbali za wanyamapori wazuri wa Australia.
-
Taarifa ya Habari 15 Septemba 2025
15/09/2025 Duración: 05minBenki ya ANZ imekiri kujihusisha na mwenendo usiofaa, katika huduma iliyotoa kwa serikali ya Australia, kulingana na Tume ya Uwekezaji na usalama ya Australia (ASIC).
-
Mutamba ahukumiwa kifungo cha kazi ngumu DR Congo
15/09/2025 Duración: 06minWaziri wa Sheria wa zamani wa DR Congo, Constant Mutamba amehukumiwa na mahakama mjini Kinshana kufanya kazi ngumu kwa miaka mitatu.
-
Félicien Kabuga apambana kupata nchi itakayo mpokea badala ya Rwanda
12/09/2025 Duración: 07minMshukiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda, Félicien Kabuga anakabiliana na wakati mgumu kupata nchi itakayo mpokea kwa muda kutoka gereza la The Hague, Uholanzi.