Sinopsis
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
Episodios
-
Kufeli kwa mkutano wa Luanda kwazua sintofahamu zaidi kwa usalama wa DRC
18/12/2024 Duración: 10minNini mustakabali wa eneo la mashariki ya DRC baada ya mkutano wa Luanda ambao uliitishwa na rais wa Angola kushindikana? Tarehe 15/12/2024 Rais Joao Laurenco wa Angola alikuwa amepanga kuwakutanisha marais wa DRC Félix Tshisekedi, na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame, mkutano ambao haukufanyika kwa sababu rais wa Rwanda hakuridhia kushiriki. Ruben Lukumbuka anazungumza na John Banyene wa mashirika ya kiraia mkoani Kivu Kaskazini mashariki mwa DRC na Al Haji Abdulkarim Atiki mchambuzi wa siasa za kimataifa akiwa Daresalaam Tanzania.
-
Uchaguzi mkuu wa Ghana: Chama tawala NPP kushindwa na chama cha upinzani NDC unatoa funzo gani?
12/12/2024 Duración: 10minNchini Ghana, rais wa zamani John Dramani Mahama alipata ushindi mkubwa na kumaliza uongozi wa miaka minane wa chama tawala New Patriotic Party (NPP) chake rais Nana Akufo-Addo, anayeondoka madarakani baada ya kuongoza kwa mihula miwili.
-
Umoja wa Mataifa unaadhimisha Siku 16 za Unaharakati dhidi ya Dhuluma za Kijinsia
30/11/2024 Duración: 10minSiku 16 za uanaharakati dhidi ya ukatili wa kijinsia ni kampeni inayofanyika kila mwaka kati ya Novemba 25 hadi Desemba 10. Ni kampeni ya siku 16 inayolenga kuhamasisha umma jinsi ya kukomesha ukatili dhidi ya wanawake na wasichana. Siku hiyo ilianza kuadhimishwa rasmi mwaka 1991,siku hii inaongozwa na Kituo cha kimataifa cha Wanawake tarehe 10 ilichaguliwa rasmi kuwa siku ya kilele cha maadhimisho haya ikiambatana na siku ya haki za binadamu duniani. Asante kwa kuendelea kuwa muaminifu kwa radio yako na kwa mtangazaji wako unaweza kumfollow kwa kubonyeza hapa Billy Bilali
-
Wakaazi wa jimbo la Somaliland wapiga kura kumchagua rais na wabunge
13/11/2024 Duración: 10minWakaazi wa jimbo la Somaliland, mojawapo wa êneo lililojitenga na Somalia zaidi ya miaka 30 iliyopita, tangu mwaka 2003 wamekuwa wakishiriki kwenye uchaguzi wa kumchagua rais na wabunge wao. Fursa hiyo pia imekuja Novemba tarehe 13 mwaka 2024 ambapo wapiga kura Milioni 1 waliondikishwa na Tume ya Uchaguzi ya Somaliland wanamchagua rais atakayewatumikia kwa miaka metano.Wagombea watatu wanatafuta urais wa jimbo hilo, akiwemo kiongozi wa sasa Muse Bihi Abdi, anayetaka muhula wa pili, lakini mpinzani wake mkuu ni Abdirahman Mohamed Abdullahi, maarufu kwa jina la "Irro,”.Kwenye Makala ya Wimbi la Siasa, tunajadili umuhimu wa uchaguzi wa jimbo la Somaliland na umuhimu wake, kwenye Jumuiya ya Kimataifa, wakati huu, êneo hilo linapotaka kujitawala.
-
Msumbuji : Upinzani wakataa kutambua ushindi wa Daniel Chapo
05/11/2024 Duración: 10minNchini Musumbuji maandamano yamekuwa yakishuhudiwa baada ya upinzani kukataa kutambua ushindi wa mgombea wa chama tawala Daniel Chapo. Aliyekuwa mgombea wa upinzani Venancio Mondlane, amekuwa akisisitiza kwamba alipokonywa ushindi, katika makala haya tunazama kujadili kile kinachoendelea nchini Musumbiji.Wachambuzi wa siasa za kimataifa Lugete Mussa Lugete na Felix Arego wanafafanua hali nchini Msumbiji.
-
Kenya : Bunge la Kenya lamuondoa naibu rais afisini
26/10/2024 Duración: 10minNchini Kenya bunge la kitaifa na seneti limeidhinisha kuondolewa afisini kwa naibu rais Rigathi Gachagua, kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo kueneza siasa za kikabila. Makala haya yaliandaliwa mapema.
-
Mgogoro kati ya rais na naibu wake nchini Kenya ambao ni mzozo wa kihistoria
23/10/2024 Duración: 10minHatma ya aliyekuwa naibu rais wa Kenya Rigathi Gachagua sasa utaamuliwa na mahakama baada ya mabunge yote mawili kumwondoa madarakani kwa njia ya hoja maalum Hatua ya kuondolewa Gachagua ni dhihirisho ya kuvunjika kwa uhusiano kati ya rais William Ruto na naibu wake Gachagua ,matukio ambayo si mageni nchini Kenya.
-
Maadhimisho ya mwaka mmoja wa shambulio la Hamas huko Gaza Oktoba 7 2024
09/10/2024 Duración: 10minMakala wimbi la siasa inaangazia maadhimisho ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kundi la Hamas, litekeleze shambulio baya zaidi kuwahi kutekelezwa huko Israeli, tukio ambalo lilianzisha vita ambayo imesababisha vifo kwa maelfu ya raia wa Kipalestina na maandamano duniani kote kupinga vita hiyo, wakati huu mzozo huo ukihofiwa kuenea katika mashariki ya kati. Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka na waalikwa wake
-
Visa vya utekaji na mauaji ya wanasiasa wa upinzani Afrika Mashariki
11/09/2024 Duración: 10minMakala ya Wimbi la siasa inaangazia tukio la kutekwa na kuuawa, kwa wanasiasa wa upinzani kwenye nchi za Afrika mashariki,tukio la hivi punde likiwa ni kutekwa kwa mwanasiasa mwandamizi wa chama cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema Ali Kibao, na baadaye alikutwa ameuawa, na matukio haya yanaripotiwa pia nchini Uganda na DRC. Ungana na Ruben Lukumbuka pamoja na waalikwa wake Jawadu Mohamed ni mchambuzi na mtaalamu wa siasa za Tanzania akiwa Daresalaam Tanzania, pia Frankline M wa CMD nchini Kenya.
-
Mzozo wa Ethiopia na Somalia na mchango wa jumuiay aza kikanda kutuliza hali
06/09/2024 Duración: 09min -
Amani ya Sudan bado kitendawili
28/08/2024 Duración: 10minMakala hii imeangazia hali ya kibinadamu inavyoendelea kuwa mbaya ndhini Sudan licha ya juhudi za kimataifa zinzoendelea.Nini kifanyike ili kufikia amani ya kudumu ya Sudan? kwa nini serikali imekataa kukaa meza moja na wapiganaji wa RSF? kuangazia hili, Ruben Lukumbuka anazungumza na Lugete Musa Lugete ni mchambuzi wa siasa za Kimataifa akiwa Tanzania, lakini pia Dismas Mokua mchambuzi wa masuala ya kisiasa akiwa Nairobi nchini Kenya
-
Mchango wa Jumuiya ya nchi za SADC katika kutafuta suluhu ya mzozo wa DRC
22/08/2024 Duración: 10minKaribu katika Makala Wimbi la siasa ambapo tunazungumzia Mkutano wa 44 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika uliofanyika Harare, Zimbabwe ambapo viongozi walijadili changamoto zinazolikabili kanda hilo hususan usalama mashariki mwa DRC. Wachangiaji mada ni Alhaj Mali Ali akiwa Paris Ufaransa na Andulkarim Atiki akiwa Dar es salaam Tanzania. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekabidhiwa jukumu la Unyekiti wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC.Kumbuka kutufollow @billy_bilali
-
Kauli ya rais Kagame kuhusu haja ya kuimarishwa kwa usalama wa kikanda
14/08/2024 Duración: 10minWakati wa kuapishwa kwake, Rais wa Rwanda Paul Kagame alikiri kuwepo kwa haja ya kuimarishwa zaidi kwa usalama katika nchi za Ukanda haswa katika eneo la mashariki ya DRC. Ruben Lukumbuka amezungumza na wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuhusu kauli hii.
-
Waasi wa M23 wauteka mji wa Ishasha licha ya sitisho la mapigano
08/08/2024 Duración: 10minWiki hii askari wanaofikia 100 wa DRC, walikimbilia Uganda baada ya waasi wa M23 kuuteka mji wa Ishasha ulioko mpakani na Uganda hali ambayo ilijiri wakati sitisho la mapigano lilikubaliwa kati ya DRC na Rwanda mjini Luanda Angola chini ya Upatanisho wa rais wa Angola Joao Laurenco. Kwa nini mapigano yanaendelea licha ya juhudi za kikanda na za kimataifa? Ruben Lukumbuka anazungumza na Francois Alwende, mchambuzi wa siasa za DRC akiwa Kenya, Jean Claude Bambaze, mwenyekiti wa mashirika ya kiraia wilayani Rutshuru akiwa Goma huko DRC.
-
DRC : Yatangaza mpango wake wa kupunguza idadi ya wafungwa magerezani
03/08/2024 Duración: 09minSerikali ya DRC imetangaza mpango wa kuwapunguza wafungwa katika magareza yake, ili kuondoa mrudiko katika taifa hilo. Katika makala haya wanaharakati wanajadili haki za wafungwa kutoka nchini DRC na Uganda.
-
Ufaransa : Macron afanikiwa kufungia mrengo wa kulia nje ya siasa za Ufaransa
15/07/2024 Duración: 09minNchini Ufaransa licha ya mrengo wa kushoto kuibuka na ushindi kwenye awamu ya kwanza ya uchaguzi wa wabunge, duru ya pili ilikuwa kitendawili kwao baada ya vyama vya mrengo wa ksuhoto kushirikiana na kuzuia vyama vya mrengo wa kulia kupata ushindi. Benson Wakoli anaangazia mbinu alaizotumia rais Emmanuel Macron kuvizuia vyama vya mrengo wa kulia kuibuka na ushindi.Kumsaidia kuangazia hili anaye mchambuzi wa siasa za kimataifa Mali Ali , ambaye yupo Pari Ufaransa, pamoja na Lugete Mussa Lugete akiwa nchini Tanzania eneo la Mwanza.
-
Kenya: Vijana watoa chanzo na suluhu ya ufisadi nchini mwao.
11/07/2024 Duración: 10minSerikali ya rais William Ruto ipo kwenye shinikizo kubwa kutoka kwa vijana nchini humo, wanaomtaka kuchukua hatua kali, kupambana na ufisadi. Tunaugana na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Multi Media nchini Kenya, wanaozungumzia mtazamo wao kuhusu vita dhidi ya ufisadi katika nchi yao.
-
Uchaguzi wa wabunge nchini Ufaransa na mustakabali wa ulaya
03/07/2024 Duración: 10minMakala ya wimbi la siasa imeangazia uchaguzi wa wabunge nchini Ufaransa baada ya kufanyika kwa duru ya kwanza ya uchaguzi huo jumapili iliyopita na sasa duru ya pili imepangwa kufanyika julai 07.Uchaguzi huu unaweka wapi siasa za ufaransa, nini mustakabali wa kisiasa kwenye nchi hii, iwapo chama cha mrengo wa kulia cha National Rally kitaibuka mshindi?? Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kupata mengi zaidi.
-
Nini hatima ya maandamano yanayoendelea nchini Kenya ?
26/06/2024 Duración: 11minSiku ya Jumanne, Kenya ilishuhudia maandamano makubwa kupinga mswada tata wa sheria uliopitishwa na wabunge, kuongzeza kodi.Waandamanaji wenye hasira, walivamia majengo ya Bunge jijini Nairobi na kusababisha uharibifu, huku polisi wakiwapiga risasi na kuwauwa waandamanaji.Nini itakuwa suluhu ya mzozo huu ?Tunachambua suala hili na Majeed Ali, mmoja wa vijana wanaounga mkono waandamanaji na Oponyo Akolo Eugene, kutoka Shirika la Wazalendo Movement Afrika, anayepinga maandamano.
-
Kuapishwa kwa Cyril Ramaphona na mstakabali wa serikali mpya ya Afrika kusini
21/06/2024 Duración: 10minMakala hii inaangazia mchakato wa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa huko Afrika kusini, baada ya kuapishwa kwa rais Ramaphosa huku chama tawala ANC kikitangaza kufikia makubaliano na vyama vingine, kama DA. Kudadavua hili mwandishi wetu Ruben Lukumbuka anazungumza na Lugete Musa Lugete ni mchambuzi wa siasa za kimataifa akiwa Jijini Daresalaam nchini Tanzania, pia Félix Nabel Arego, mtaalamu wa siasa wa siasa za Afrika kusini akiwa Nairobi Kenya