Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Shirika la Weather Mtaani labuni teknolojia ya kuepuka majanga ya hali ya hewa Kibera

Informações:

Sinopsis

Mvua huja kwa sauti ya baraka lakini katika kitongoji, sauti hiyo hubeba hofu. Maji yanapoteremka kutoka angani, katika sekunde chache, barabara hugeuka mito. Vyumba vya kulala vinageuka mabwawa. Katika kitongoji cha Kibera jijini Nairobi nchini Kenya, hali hiyo ya hofu imebadilishwa kupitia kundi la vijana linalojiita Weather Mtaani. Shirika la Weather Mtaani linatumia teknolojia ya simu kutafsiri jumbe za utabiri wa hali ya hewa kutoka kwa mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa ya Kenya, kwa lugha inayoeleweka.