Habari Za Un
07 APRILI 2025
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:11:47
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Hii leo jaridani tunaangazia makumbusho ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, na Siku ya Afya Duniani. Makala inamulika nafasi ya michezo katika kusongesha amani na maendeleo, na mashinani tunakwenda nchini Kenya, kulikoni?Dunia inapokumbuka miaka 31 tangu mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma ujumbe mzito wa maombolezo na onyo, akitaka mshikamano wa kimataifa kupambana na ongezeko la chuki, mgawanyiko, na misimamo mikali kupitia mifumo ya kidijitali.Leo ni Siku ya Afya Duniani ambayo mwaka huu inangazia suala muhimu kwa afya ya dunia, changamoto maalum wanazokumbana nazo wanawake na wasichana lakini pia vifo vya watoto wachanga, na ili kuhakikisha changamoto hizo zinashughulikiwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO limezindua kampeni ya mwaka mzima ya “Mwanzo wenye afya ni mustakbali wenye matumaini”..Makala inamulika nafasi ya michezo katika kusongesha amani na maendeleo, ambapo Assump