Habari Za Un

Dayspring Foundation nchini Tanzania yatekeleza kivitendo dhana ya UN ya michezo kwa maendeleo

Informações:

Sinopsis

Siku ya kimataifa ya Michezo kwa ajili ya Maendeleo na Amani imeadhimishwa tarehe 6 mwezi huu wa Aprili maudhui yakiwa Ujumuishaji wa kijamii, hususan makundi ya pembezoni. Umoja wa Mataifa kupitia wavuti wake unasema kuwa siku hii inatambuliwa kutokana na nafasi ya michezo katika kuleta mabadiliko chanya, kuondoa vikwazo na kuvuka mipaka. Na usuli wa maudhui ya mwaka huu ni kwamba fikra potofu kwenye jamii zimesababisha baadhi ya watu kutokana na jinsia yao, umri, au rangi wanashindwa kushiriki kwenye michezo ambayo kwa njia moja au nyingine hutokomeza umaskini kwa kuwezesha washiriki kujipatia kipato. Nchini Tanzania shirika la kiraia la Dayspring Foundation limetambua nafasi ya michezo na limeanza kuchukua hatua. Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Rosemary Mwaipopo ambaye anaanza kwa kuelezea ni kwa nini waliamua kujikita katika kusaka vipaji.