Habari Za Un

Wanachama wa WHO wachukua hatua za kujenga uwezo dhidi ya majanga yajayo ya afya

Informações:

Sinopsis

Baada ya zaidi ya miaka mitatu ya mazungumzo ya kina, hatimaye leo Geneva, Uswisi, Nchi Wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) zimekamilisha rasimu ya makubaliano ambayo itawasilishwa katika Mkutano wa Afya Duniani mwezi Mei mwaka huu wa 2025. Pendekezo hili linakusudia kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na vitisho vya majanga ya kiafya yajayo. Anold Kayanda amefuatilia anatujulisha zaidi.  "Leo mataifa ya dunia yameandika historia mjini Geneva," amesema Dkt. Tedros Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO na kuongeza kwamba, "kwa kufikia makubaliano kuhusu Mkataba wa Majanga ya kiafya, siyo tu wameweka msingi wa makubaliano ya kizazi hiki yanayolenga kuifanya dunia kuwa salama zaidi, bali pia wameonesha kuwa ushirikiano wa kimataifa bado uko hai, na kwamba hata katika dunia iliyogawanyika, mataifa bado yanaweza kushirikiana kutafuta mwafaka na mwitikio wa pamoja dhidi ya vitisho vya pamoja.” Mwezi Desemba mwaka 2021, wakati janga la C