Afrika Ya Mashariki
Athari za mgogoro wa DRC katika mataifa ya Afrika
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:09:42
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Mgogoro wa Mashariki ya DRC umeendelea kwa miongo kadhaa, na bado ni moja ya changamoto kubwa za kiusalama na kisiasa Barani Afrika. Katika Mashariki ya DRC, kuna makundi ya waasi kama vile M23, ADF, Twirwaneho, ambayo yameongeza umwagaji damu na kusababisha maelfu ya watu kuhama kutoka maeneo yao.Siasa za kikanda, ushindani wa madaraka kati ya mataifa kama Rwanda yana iweka DRC njia panda kila uchao Karibu katika Makala ya Afrika mashariki hii tunangaza mgogoro mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mwandalizi na msimulizi wako naitwa Martin Nyoni nasema karibu tuwe sote hadi tamati Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kibinadamu, hasa katika majimbo ya mashariki ya Ituri, Kivu Kaskazini, Kivu Kusini na Tanganyika, kutokana na migogoro ya silaha na mapigano baina ya jamii. Mnamo Septemba 2024, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM)