Afrika Ya Mashariki
Umuhimu wa kutunza lugha mama katika jamii za Afrika
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:09:59
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Karibu katika Makala ya Afrika mashariki hii leo tukiangaza safari ya miaka 25 ya UNESCO kuenzi lugha mama na nafasi ya lugha mama katika kukuza maendeleo ya jamii Mwandalizi na msimulizi wako naitwa Martin Nyoni nasema karibu tuwe sote hadi tamati ya Makala haya. Lugha ni muhimu kwa elimu na maendeleo endelevu, zikitumika kama njia kuu ambayo maarifa hupitishwa na tamaduni kuhifadhiwa. Kwa mujibu wa taarifa iliyo chapishwa katika tovuti ya Umoja wa mataifa inaeleza kukiwa na takriban lugha 8,324 duniani leo, nyingi ziko hatarini kutoweka kutokana na utandawazi na mabadiliko ya jamii.Kuhakikisha kwamba mifumo ya elimu inaunga mkono haki ya mtu ya kujifunza katika lugha-mama ni muhimu sana katika kuboresha matokeo ya kujifunza, kwani wanafunzi wanaofundishwa kwa lugha wanayoelewa kikamilifu huonyesha ufahamu bora, ushirikishwaji, na ustadi wa kufikiri kwa kina.