Habari Za Un

Huu ni wakati wa kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na AI-Guterres

Informações:

Sinopsis

Viongozi wa kimataifa wa masuala ya kisiasa na biashara wanaokutana Davos Uswisi kwa ajili ya jukwaa la kiuchumi duniani WEF, leo wamekabiliwa na ukweli mchungu kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, akilaani ukosefu wa ushirikiano wa kimataifa katika dunia inayokosa mwelekeo, ikikabiliwa na hatari mbili kubwa ambazo ni mabadiliko ya tabianchi na akili mnemba au AI isiyodhibitiwa. Flora Nducha na taarifa zaidiAkizungumza katika Jukwaa hilo la kila mwaka la Kiuchumi Duniani Katibu Mkuu amewaonya viongozi wa dunia na wakuu wa biashara kuhusu vitisho viwili vinavyoongezeka kwa ubinadamu mabadiliko ya tabianchi na akili mnemba au AI isiodhibitiwa amesema “Kunapokuja suala la tishio la kimataifa nyuklia sio tishio pekee. Leo hii tunakabiliwa na matishio mawili makubwa ambayo yanahitaji kupewa uziti Mkubwa wa kimataifa na hatua kwa sababu yanatishia kubadili kabisa maisha tunayoyajua, janga la mabadiliko ya tabianchi na upanuzi wa kasi wa wigo wa akili mnemba.”Akikosoa ukosefu wa ushiriki