Wimbi La Siasa

Kufeli kwa mkutano wa Luanda kwazua sintofahamu zaidi kwa usalama wa DRC

Informações:

Sinopsis

Nini mustakabali wa eneo la mashariki ya DRC baada ya mkutano wa Luanda ambao uliitishwa na rais wa Angola kushindikana? Tarehe 15/12/2024 Rais Joao Laurenco wa Angola alikuwa amepanga kuwakutanisha marais wa DRC Félix Tshisekedi, na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame, mkutano ambao haukufanyika kwa sababu rais wa Rwanda hakuridhia kushiriki. Ruben Lukumbuka anazungumza na John Banyene wa mashirika ya kiraia mkoani Kivu Kaskazini mashariki mwa DRC na Al Haji Abdulkarim Atiki mchambuzi wa siasa za kimataifa akiwa Daresalaam Tanzania.