Sinopsis
Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.
Episodios
-
Riadha: Ni nani atashinda mbio za London Marathon mwaka 2025?
26/04/2025 Duración: 24minLeo tumeangazia michuano ya klabu bingwa kufuzu fainali, riadha za Diamond League, Boston na London Marathon, Cameroon yafuzu Kombe la Dunia la U17, uchaguzi wa kamati ya Olimpiki nchini Kenya watibuka, Gor Mahia yanuia kujenga uwanja wao, uchambuzi wa debi ya El Clasico huku Carlos Alcaraz akijiondoa kwenye mashindano ya Madrid Open.
-
Jean-Jacques wa DRC kati ya waamuzi waliochaguliwa kwenye Kombe la Dunia la Vilabu
19/04/2025 Duración: 23minJumamosi hii tunaangazia nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika, waamuzi kutoka Kenya na DRC miongoni mwa waamuzi kusimamia michuano ya Kombe la Dunia la Vilabu Marekani mwaka huu, fainali wa Afcon U17, kwenye riadha Chepngetich na Jepchirchir wajiondoa kwenye London Marathon, mechi za kufuzu Kombe la Dunia la wasichana chini ya umri wa miaka 17 pamoja uchambuzi wa robo fainali tatanishi kwenye ligi za mabingwa ulaya wiki hii.
-
CAF: Simba yatinga nusu fainali michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika
12/04/2025 Duración: 24minTuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa matokeo ya robo fainali mechi za klabu bingwa Afrika, Uganda yalenda kufuzu Kombe la Dunia wasiozidi miaka 17, timu ya taifa ya raga ya kina dada ya Kenya yalenga kurejea katika msururu wa dunia, michuano ya vilabu ya Afrika mchezo wa voliboli, Rwanda yaadhimisha miaka 31 michezoni tangu mauaji ya kimbari, Maluki atangaza nia ya kuwania urais wa Nock, Salah asaini kandarasi mpya Liverpool, Real Madrid itageuza meza dhidi ya Arsenal?
-
Raga: Nafasi ya Shujaa 7s kusalia kwenye msururu wa raga duniani ni gani?
05/04/2025 Duración: 23minLeo kwenye kipindi tumeangazia mkondo wa kwanza robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika, matokeo ya Uganda na Tanzania kwenye michuano ya AFCON U17 huk Morocco, nafasi ya Shujaa 7s ya Kenya kusalia kwenye msururu wa raga duniani, mnyarwanda Celestine Nsanzuwera ashinda michuano ya gofu ya Sunshine Tour Afrika Mashariki, wachezaji watano wa ufaransa wa tenisi wapokea adhabu kwa makosa ya upangaji matokeo, Muller na De Bruyne kuondoka vilabuni mwao mwishoni mwa msimu huu.