Sinopsis
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.
Episodios
-
Wanaharakati wa Kenya na Uganda wajieleza, Rais wa DRC akutana na mpinzani Martin Fayulu
07/06/2025 Duración: 20minWito wa wanaharakati wa haki za binadamu kwa serikali za Kenya na Tanzania, kuwashughulikia maafisa wa polisi waliowatendea dhulma na unyanyasaji wa kijinsia, mkutano kati ya rais wa DRC Félix Tshisekedi na mwanasiasa wa upinzani na kiongozi wa chama cha Ecidé Martin Fayulu, siasa za Uganda, Kenya maeneo ya afrika magharibi na kati na pia katika mataifa mengine
-
Rais mstaafu wa DRC Joseph Kabila mjini Goma, Ngugi wa Thiongo aaga dunia
07/06/2025 Duración: 19minMakala ya wiki hii hadi mei 31 imeangazia kuwasili kwa rais mstaafu wa DR Congo Joseph Kabila katika mji wa Goma, kifo cha gwiji wa fasihi raia wa Kenya Ngugi wa Thiong'o kule Marekani, ripoti ya shirika la Amnesty International yasema zaidi ya watu elfu kumi waliuawa nchini Nigeria katika kipindi cha miaka miwili, Sidi Ould Tah kutoka Mauritania ndiye rais mpya wa Benki ya maendeleo ya Afrika, na Israeli kujenga makazi mapya katika ukingo wa Jordan.Ungana na mwandishi wetu Emmanuel Makundi
-
Kabila aondolewa kinga ya kushtakiwa na Seneti ya DRC, Lissu arejeshwa mahakamani Tanzania
29/05/2025 Duración: 20minMiongoni mwa taarifa utakazoziskia ni pamoja na; Bunge la seneti nchini DRC lapiga kura ya kumuondolea kinga rais mtaafu Joseph kabila, Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu na Mawakili mashuhuri kutoka nchini Kenya, wafukuzwa nchini Tanzania. Kwingineko, Mamlaka nchini Libya zagundua miili 58 iliohifadhiwa kwa muda katika chumba cha kuhifadhi maiti na Waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu awatuhumu viongozi wa Ufaransa, Uingereza na Canada kwa kuwapa nguvu kundi la Hamas.
-
DRC: Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki wamtaka Rais Felix Tshisekedi kuwaamini viongozi wa dini
22/05/2025 Duración: 20minMakala haya yanaangazia taarifa mbalimbali ikiwemo, Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini DRC wamtaka Rais Felix Tshisekedi kuwaamini viongozi wa dini kusaidia kuleta amani na utulivu Mashariki mwa nchi hiyo na pia serikali ya Uganda yawasilisha mswada tata bungeni kuruhusu kesi za kiraia kupelekwa kwenye Mahakama ya kijeshi. Taarifa zingine ambazo utaziskia ni uongozi wa kijeshi nchini Mali wasitisha sheria kuhusu vyama vya siasa nchini humo na Mazungumzo ya ana kwa ana kati ya wajumbe wa Ukraine na Urusi yamefanyika wiki hii nchini Uturuki kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2022.