Sinopsis
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.
Episodios
-
Tanzania: Wiki hii tunaliangazia kundi la Muziki la The Mafiki
24/08/2024 Duración: 20minThe Mafiki ni kundi la Muziki lililovuma kwa vionjo vya Muziki wa sasa, sasa wamekuja upya mara baada ya kusambaratika, Ungana na Steven Mumbi akizungumza na wasanii wa kundi hilo.
-
Muziki wa Taarab nchini Tanzania naye Jike la Chui
17/08/2024 Duración: 20minMapinduzi ya Muziki wa Taarab yanajidhihirisha katika tenzi za wasanii wa Muziki huu kutoka tungo za Majigambo na sasa tungo za kuburudisha, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Jike la Chui.
-
Zumbukuku nyimbo za taarab zinazokumbukwa hata sasa
03/08/2024 Duración: 20minZumbukuku ni miongoni mwa nyimbo zilizofanya vizuri katika muziki wa taarab, hii inashehenezwa na sauti ya kipekee ya kiume inayosikika katika muziki huo, Ally Star ndie aliyeimba wimbo huo; Ungana na Steven Mumbi katika makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Ally Star kuhusu namna nyimbo hizo zilivyotia fora.
-
Mwanamuziki Ogisha Matale atoa wito wa amani mashariki mwa DRC
27/07/2024 Duración: 20minMakala ya nyumba ya sanaa wiki hii imepiga kambi mjini Goma huko mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ambako mwanzoni mwa mwezi mei mwandishi wetu Ruben Lukumbuka alikutana na msanii Ogisha Matale ambapo katika shughuli zake zake amekuwa akijaribu kuhimiza amani nchini, hususan eneo lake lenye kushuhudia mapigano ya mara kwa mara.